Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 15:16
VOA Direct Packages

Kiongozi wa LGBTQ nchini Uganda ahofia kupoteza makazi yake


Wabunge wa Uganda wakipitisha mswaada wa sheria kali dhidi ya jamii ya LGBTQ mapema wiki hii.
Wabunge wa Uganda wakipitisha mswaada wa sheria kali dhidi ya jamii ya LGBTQ mapema wiki hii.

Kiongozi mashuhuri wa jamii ya wapenzi wa jinsia moja nchini Uganda Alhamisi amesema kwamba anahofia kukosa makazi akielezea matatizo yanayokumbwa wenzake pia.

Hali hiyo imejitokeza baada ya mswada wa sheria kali dhidi ya LGBTQ kupitishwa na bunge wiki hii. Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, Frank Mugisha ambaye ni kiongozi wa kundi lililopigwa marufuku nchini humo la Sexual Monorities of Uganda amesema kwamba anahofia kufurushwa kutoka nyumba anayopanga, na kwa hivyo kubaki bila makao kwa kuwa hana sehemu yake anayomiliki.

Mugisha aliyasema hayo kwa AP wakati shinikizo liliendelea kuongezeka kutoka Marekani na Umoja wa Mataifa, kwa rais Yoweri Museveni kutotia saini mswaada huo uliopitishwa na bunge Jumanne. Mswaada huo unapendekeza hukumu ya kifo kwa ushoga wa kulazimishwa na kifungo cha maisha kwa wapenzi wa jinsia moja. Ushoga wa kulazimishwa ni ule kati ya watu wenye maradhi ya HIV, watoto au watu wasioweza kujilinda wenyewe. Haijabainika ni lini Museveni atakapo fahamisha bunge hususu uamuzi wake.

XS
SM
MD
LG