Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:15

Wakimbizi Uganda wakabiliwa na uhaba wa mboga za majani


Wakimbizi kutoka DRC wakipata chakula cha mchana huko Kisoro, Uganda, tarehe 7 Juni, 2022. Picha na BADRU KATUMBA/AFP.
Wakimbizi kutoka DRC wakipata chakula cha mchana huko Kisoro, Uganda, tarehe 7 Juni, 2022. Picha na BADRU KATUMBA/AFP.

Akiwamgilia maji kwenye matuta nadhifu yaliyojipanga kwa mstari yenye mboga za majani nje ya nyumba ya nyasi ya Susan Konga, mwanamke raia wa Sudan Kusini ambaye anaishi katika kambi ya wakimbizi iliyoko kaskazini mwa Uganda, anaiandaa bustani yake ya mboga kwa ajili ya msimu ujayo wa mavuno.

Mwaka huu mafanikio ya juhudi zake katika kilimo yatakuwa ni mtihani - kujitosheleza kikamilifu. Migogoro ya kimataifa kama vile vita vya Ukraine, tetemeko la ardhi nchini Uturuki na ukame katika maeneo ya Afrika Mashariki, inamaanisha misaada michache ya chakula kwa mtu kama Konga.

Upungufu wa asilimia 50 wa ufadhili mwaka huu umelilazimisha shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kupunguza usambazaji wa chakula kwa maelfu ya wakimbizi nchini Uganda, ambayo ni mwenyeji wa wakimbizi wengi zaidi kuliko nchi yoyote barani Afrika.

Baada ya kuishi miaka sita nchini Uganda, Konga, mwanamke ambaye hana mume, hivi sasa hana budi kutegemea mahindi, mihogo na mboga za majani anazolima kwenye bustani yake ndogo. Mabadiliko ya sera yatamletea ugumu kuzoea, amesema.

Konga ana wasiwasi kuwa hataweza kulima chakula cha kutosha na kuwa na ziada ya kuuzaa ili aweze kumudu ada za shule kwa wapwa zake wawili pamoja na kununua mahitaji mengine ya msingi ya nyumbani kama vile sabuni.

"Kwangu mimi kuwa endelevu itanichukua zaidi ya miaka mitatu, kwa sababu kwa sasa sina ardhi ya kutosha," alisema. "kama sipati msaada, siwezi kusimama mwenyewe."

WFP linasema wakimbizi walio katika mazingira hatarishi kama wale wapya wanaowasili, wagonjwa na wazee, wataendelea kupatiwa misaada ya dharura ya chakula, lakini shirika hilo lina upungufu wa dola milioni 180 hii inamaanisha kuwa wengine waondolewe katika kupokea misaada.

XS
SM
MD
LG