Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:15

Mtoto wa Rais Museveni asema Uganda itatuma wanajeshi kuilinda Moscow


Mtoto wa Rais Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba
Mtoto wa Rais Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba

Mtoto wa kiume wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni Alhamisi alitangaza kwamba nchi yake itatuma wanajeshi kuulinda mji wa Moscow ikiwa utakabiliwa na tishio.

“Niite mfuasi wa Putin ukipenda, lakini sisi, Uganda tutatuma wanajeshi kuilinda Moscow ikiwa itatishiwa na mabeberu, “Muhoozi Kainerugaba alisema kwenye Twitter.

Jenerali huyo wa jeshi ambaye ni mfwasi mkubwa wa Rais wa Russia Vladimir Putin ameongeza kuwa “ Nchi za magharibi zinapoteza muda wake na propaganda zisizo na maana za kuiunga mkono Ukraine.”

Kainerugaba ambaye amepata umaarufu mkubwa kwenye mtandao wa Twitter kutokana na maoni yake kuhusu masuala mbalimbali, mapema mwezi huu alitangaza kwamba anapanga kuwania urais kwenye uchaguzi wa 2026.

Jana, alitangaza pia kuwa ataanzisha kituo cha televisheni na radio chini ya chapa yake ya MK, na amesema mmoja ya maeneo ya kwanza atakayotembelea itakuwa Russia.

XS
SM
MD
LG