Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 23:39

Wanariadha 50 wapiga mbizi Mto Seine baada ya kuhakikishiwa maji yake salama


Paris Olympics Triathlon
Paris Olympics Triathlon

Zaidi ya wanariadha wanawake 50 walipiga mbizi  katika Mto Seine Jumatano asubuhi saa kadhaa baada ya waandaaji wa michezo ya Olimpiki Paris kusema kuwa ubora wa maji ulikuwa siyo hatari kwa kuogelea.

Eneo la kuogelea katika michezo hiyo lilitiliwa mashaka kwa siku kadhaa baada ya vipimo kuonyesha viwango vya juu vya bakteria katika mkondo wa maji kutokana na mvua zilizonyesha mwishoni mwa wiki, na kuwaweka waogeleaji katika hatari ya maambukizi.

Hali hiyo iliwalazimisha waandaaji kufuta vipindi viwili vya mafunzo na kuahirisha uogeleaji wa wanaume Jumanne.

Uogeleaji kwa Triathlon

Waandaaji wanafikiria kufuta sehemu ya uogeleaji kwa triathlon ambapo wanawake wanashiriki kama viwango vya bakteria vitakuwa bado vitakuwa juu mno, na kuwaacha washiriki katika mashindano ya baskeli na kukimbia.

Lakini hatari ya kweli inatokana na utelezi wa barabara baada ya mvua za mapema asubuhi, zikisababisha wanariadha kadhaa kuteleza na kuanguka wakati wa mashindano ya baiskeli.

Cassandre Beaugrande

Mashindano kamili ya mbio yalifanyika na Cassandre Beaugrande wa Ufaransa alishinda medali ya dhahabu baada ya kumaliza mbio hizo kwa kuvuka mstari katika daraja la kihistoria la Alexandre III kwa saa moja na dakika 54 na sekunde 55.

Beaugrande alimshinda mshindi wa medali ya fedha Julie Derron wa Uswizi kwa sekunde sita, huku mwanariadha wa Uingereza Beth Potter akishinda medali ya shaba.

Saa kadhaa baada ya kumaliza mbio za wanawake, mashindano ya wanaume yanayohusisha michezo mitatu (kuogelea, baiskeli na mbio) huku Muingereza Alex Yee akishinda medali ya dhahabu kwa kutumia saa moja, dakika 43 na sekunde 33.

Hayden Wilde

Mwanariadha wa New Zealand Hayden Wilde alimaliza mbio hizo sekunde sita baadaye na kushinda medali ya fedha, huku washangiliaji wa Paris wakimshangilia mtoto wa nyumbani Leo Bergere kwa kushinda medali ya shaba.

Kuongelea katika Mto Siene unaojulikana kwa uchafu kulipigwa marufuku kwa zaidi ya karne moja.

Paris imetumia dola bilioni 1.5 tangu mwaka 2015 kujenga miradi ya miundombinu mipya kuusafisha mto huo kwa ajili ya michezo ya Olimpiki.

Meya Anne Hidalgo aliogelea katika Mto Seine wiki kadhaa zilizopita kuonyesha kuwa hali yam to huo ni salama kwa wanariadha na wakazi wa Paris wakati Michezo hiyo ikimalizika.

Baadhi ya taarifa hii inatokana na ripoti za mashirika ya habari ya Some information The Associated Press, Reuters, Agence France-Presse.

Forum

XS
SM
MD
LG