Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 23:12

Wanafunzi watano wa kike watekwa nyara Nigeria


Wasichana waliokuwa wametekwa nyara kutoka shule ya bweni iliyoko Kaskazini-Magharibi mwa jimbo la Zamfara huko Nigeria, wakipanda gari baada ya kuachiliwa Machi 2, 2021. Picha na REUTERS/Afolabi Sotunde
Wasichana waliokuwa wametekwa nyara kutoka shule ya bweni iliyoko Kaskazini-Magharibi mwa jimbo la Zamfara huko Nigeria, wakipanda gari baada ya kuachiliwa Machi 2, 2021. Picha na REUTERS/Afolabi Sotunde

Watu wenye silaha wamewateka nyara wanafunzi watano kaskazini mwa Nigeria, polisi walisema, siku chache baada ya wanafunzi wengine zaidi ya 20 kutekwa nyara katika eneo lililoko jirani.

Operesheni ya polisi inaendelea ya kuwatafuta wanafunzi hao watano wa kike, waliotekwa nyara siku ya Jumatano, walisema polisi.

Mtu mmoja amezuiliwa.

"Majira ya saa nane usiku, washukiwa wa ugaidi waliwateka nyara wanafunzi watano wa kike wa chuo kikuu cha serikali," Aliyu Abubakar Sadiq, msemaji wa polisi katika jimbo la Katsina, alisema katika taarifa iliyotolewa Jumatano jioni.

Tukio hilo limetokea chini ya wiki mbili baada ya watu wenye silaha kutoka kwenye magenge ya "majambazi" ya wahalifu kuwateka nyara zaidi ya watu 30, wakiwemo wanafunzi wasiopungua 24 wa kike, katika uvamizi kuzunguka chuo kikuu kilichokuwa nje ya mji mkuu wa Gusau, ulioko katika jimbo la Zamfara.

Wanajeshi wa Nigeria wamewaokoa mateka 16 wakiwemo wanafunzi 13.

Uvamizi huo ulikuwa utekeji nyara wa kwanza wa watu wengi katika chuo kimoja tangu Rais Bola Ahmed Tinubu aingie madarakani mwezi Mei, Tinubu aliahidi kukabiliana na ukosefu wa usalama nchini Nigeria, ambako magenge ya utekaji nyara kwa ajili ya fidia yamekuwa yakifanya mashambuzi ya mara kwa mara mashuleni.

Chanzo cha habari ni Shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG