Akizungumza kwenye televisheni ya taifa kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa nchi yake, tangazo la Tinubu limekuja baada ya kuondoa ruzuku ya muda mrefu ya mafuta ambayo iliigharimu serikali mabilioni ya dola kwa mwaka na kuifanya biashara huria ya sarafu ya naira.
Maafisa wa serikali wanasema mageuzi hayo yalikuwa yanahitajika ili kufufua uchumi wa taifa hilo na wawekezaji walipongeza mageuzi hayo, lakini Wanigeria wanasumbuka na kupanda mara tatu kwa bei ya mafuta na mfumuko wa bei ambao umefikia sasa asilimia 25.
Forum