Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 22:34

Wanafunzi wa Chuo Kikuu watekwa nyara Nigeria


Rais wa Nigeria Bola Tinubu alipokuwa katika mkutano wa mwisho wa kampeni za uchaguzi huko Lagos, Februari 21 2023. Picha na REUTERS/Nyancho Nwanri.
Rais wa Nigeria Bola Tinubu alipokuwa katika mkutano wa mwisho wa kampeni za uchaguzi huko Lagos, Februari 21 2023. Picha na REUTERS/Nyancho Nwanri.

Watu wenye bunduki wamewateka nyara watu 35 kutoka chuo kikuu kilichopo kaskazini magharibi katika Jimbo la Zamfara nchini Nigeria, msemaji wa gavana Mugira Yusuf alisema, huu ni utekaji nyara mkubwa wa kwanza mwaka huu uliowahusisha wanafunzi

Msemaji wa gavana, alisema wanafunzi 24, wafanyakazi 10 na mlinzi walikamatwa na watu wenye silaha siku ya Ijumaa alfajiri kutoka Chuo Kikuu cha Federal of Gusau.

Magenge yenye silaha yamekuwa yakishambulia eneo la kaskazini magharibi katika miaka ya hivi karibuni, utekaji nyara kwa ajili ya fidia, uporaji na uharibifu katika jamii na mauaji ya raia. Majaribio ya majeshi ya usalama kusitisha vurugu hizo yamekuwa na mafanikio kidogo.

Wanajeshi waliwaokoa wanafunzi sita wa kike na kuwaua watekaji nyara watano wakati walipokuwa wakirushiana risasi, chanzo cha usalama kilisema.

Chanzo hicho pia kilisema, operesheni ya pamoja ya usalama kati ya jeshi na polisi ilikuwa ikiendelea ili kuachiliwa huru wale ambao walikuwa bado wamekamatwa.

Utekaji nyara wa wanafunzi, ambayo hapo awali ilikuwa mbinu mbaya iliyokuwa ikitumiwa na kundi la wanamgambo wa kiislamu ambao walikuwa wakiwatishia watu, imekuwa chanzo cha kuingiza pesa kwa magenge yenye silaha yanayodai fidia.

Rais Bola Tinubu aliahidi kumaliza ukosefu wa usalama ulioenea wakati wa kampeni zake za uchaguzi mapema mwaka huu, lakini bado hajaeleza jinsi atakavyotatua tatizo hilo.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG