Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 18:52

Mahakama ya Nigeria yatupilia mbali ombi la chama cha upinzani la kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa rais


Rais wa Nigeria Bola Tinubu wakati wa hafla ya kuapishwa mjini Abuja, Mei 29, 2023.
Rais wa Nigeria Bola Tinubu wakati wa hafla ya kuapishwa mjini Abuja, Mei 29, 2023.

Mahakama ya rufaa ya Nigeria leo Jumatano imetupilia mbali ombi la moja kati ya vyama viwili vya upinzani kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwezi Februari, ulioshindwa na Bola Tinubu ambaye yuko madarakani tangu mwezi Mei.

Majaji watano wa Mahakama ya Abuja wamekuwa wakijadiliana kwa miezi kadhaa kesi za vyama vya upinzani vya Peoples Democratic Party (PDP) na Labour Party vinavyodai kwamba uchaguzi uligubikwa na udanganyifu na kasoro.

Madai ya chama cha Labour kwamba kulikuwa na kasoro zilizojitokeza katika mamlaka ya uchaguzi, wizi wa kura na madai kwamba Tinubu hakustahili kugombea, yametupiliwa mbali na mahakama.

Uamuzi kuhusu ombi la chama cha PDP ulikuwa bado ukisubiriwa.

Katika kinyang’anyiro chenye upinzani mkali, gavana wa zamani wa Lagos Tinubu alipata asilimia 37 ya kura katika uchaguzi wa Februari 25, akiwashinda Atiku Abubakar wa PDP na Peter Obi wa chama cha Labour na kupata urais katika taifa hilo lenye watu wengi barani Afrika.

Wanasheria wanasema uamuzi wowote utakaochukuliwa bado utawasilishwa kwenye mahakama ya juu kwa ajili ya uamuzi wa mwisho.

Forum

XS
SM
MD
LG