Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 14:36

Nigeria yakosa umeme


Moja ya eneo la jiji la Lagos, ambalo ni kitovu cha biashara cha Nigeria, Picha na REUTERS/George Esiri GE/CRB
Moja ya eneo la jiji la Lagos, ambalo ni kitovu cha biashara cha Nigeria, Picha na REUTERS/George Esiri GE/CRB

Makampuni ya usambazaji umeme nchini Nigeria yameripoti "kuvunjika kabisa kwa mfumo" wa uzalishaji umeme siku ya Alhamisi, na kusababisha umeme kukatika katika maeneo mbalimbali kwenye taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika.

Siku ya Alhamisi baada ya moto kutokea kwenye njia kuu ya kusambaza umeme, ilisababisha umeme kukatika kote katika taifa hilo.

Waziri wa nishati Adebayo Adelabu, alisema moto ulisababisha mlipuko kwenye njia ya usambazaji umeme inayounganisha mitambo ya Kainji na Jebba katika jimbo la kaskazini la Niger, na kutegua gridi ya taifa.

"Moto huo umedhibitiwa kabisa na zaidi ya nusu ya

Njia za kuungaisha sasa zinafanyakazi na muda mfupi ujao huduma kamili zitarejeshwa kote," Adelabu alisema katika taarifa.

Uzalishaji umeme ulishuka hadi sifuri katika nyakati za asubuhi na kupanda tena baadaye hadi megawati 273, lakini kiwango hicho bado ni chini ya wastani wa usambazaji wa siku wa Megawati 4,100, data kutoka kwa Kampuni ya Usambazaji ya Nigeria (TCN) ilionyesha.

Usambazaji wa umeme wa gridi ya taifa umekuwa ukisuasua nchini Nigeria, ambayo ni mzalishaji mkubwa ya mafuta na gesi, na kuzilazimisha kaya na biashara kutumia dizeli na mafuta kwa ajili ya majenereta.

Mwaka 2022 , Gridi hiyo ya umeme imeshindwa kufanya kazi angalau mara nne, ambapo mamlaka zimekuwa zikilaumu matatizo ya kiufundi.

Nigeria ina MW 12,500 za uwezo uliowekwa lakini inazalisha

takriban robo ya kiwangio hicho. Rais Bola Tinubu ameahidi kuboresha usambazaji kwa kuruhusu serikali za majimbo kujenga mitambo yao ya kuzalisha umeme kwa nia ya kusaidia kuchochea ukuaji duni wa uchumi.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG