Nigeria nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika na taifa lenye uchumi mkubwa barani Afrika, inafikiria kuomba kujiunga na kundi la mataifa ya G20, Rais wa nchi hiyo amesema.
Rais Bola Ahmed Tinubu ambaye aliingia madarakani mwezi Mei anapanga kuhudhuria mkutano wa G20 nchini India wiki hii ambapo masuala ya biashara, uchumi wa dunia, hali ya hewa na vita vya Ukraine yatakuwa kwenye ajenda.
Tangu achukue urais, Tinubu ameanzisha mageuzi makubwa ambayo serikali yake inasema yatarudisha uchumi wa Nigeria katika njia nzuri na pia kuvutia uwekezaji wa kigeni unaohitajika sana. Katika taarifa siku ya Jumapili, msemaji wa rais Ajuri Ngelale alisema kwamba uanachama wa G20 ulikuwa unahitajika, lakini serikali ilikuwa katika majadiliano kutathmini faida za kujiunga na kundi hilo.
Mara baada ya mashauriano kukamilika serikali itaamua ikiwa itaomba kujiunga au la kama ikibidi, ilisema. Ushiriki wa Rais Tinubu katika Mkutano wa G20 nchini India, kwa sehemu, ni katika kuendeleza lengo hili.
Forum