Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 19:13

Wakenya wafungwa miaka 20 Uganda


Mfugaji wa kabila la Karamojong akichunga mbele ya Mlima Moroto huko Uganda jirani na mpaka wa Kenya. Picha na Luis TATO / FAO / AFP.
Mfugaji wa kabila la Karamojong akichunga mbele ya Mlima Moroto huko Uganda jirani na mpaka wa Kenya. Picha na Luis TATO / FAO / AFP.

Mahakama ya kijeshi nchini Uganda imewahukumu dazerni ya wafugaji kutoka Kenya kifungo cha miaka 20 jela, baada ya kukiri kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria, afisa mmoja alisema Alhamisi.

Wafugaji hao 32 kutoka eneo la kaskazini mwa Kenya walikamatwa katika operesheni ya kijasusi siku ya Jumamosi, kufuatia mapambano ya risasi katika wilaya ya Moroto kaskazini mashariki mwa Uganda, Brigedia Jenerali Joseph Balikuddembe aliliiambia shirika la habari la AFP.

Watuhumiwa hao walifikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi siku ya Jumanne, afisa huyo wa Moroto alisema.

"Washukiwa 32... walikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka 20, baada ya kukubali kosa la kukutwa na silaha pamoja na risasi kinyume cha sheria," alisema.

Eneo hilo lililojitenga na maskini lililoko kaskazini-mashariki mwa nchi limevumilia miongo kadhaa ya visasi vya uvamizi wa ng'ombe unaofanywa na watu wenye silaha wa koo za wahamaji ambao wanazunguka maeneo yasiyokuwa na sheria yaliyoko kati ya Uganda, Sudan Kusini na Kenya.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari ka AFP.

XS
SM
MD
LG