Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 18:49

Wabunge wa Ruto kukutana na Upinzani



Rais William Ruto, alipowasili katika majengo ya bunge jijini Nairobi, tarehe 29 Septemba 29, 2022. Picha na Simon MAINA/AFP.
Rais William Ruto, alipowasili katika majengo ya bunge jijini Nairobi, tarehe 29 Septemba 29, 2022. Picha na Simon MAINA/AFP.

Serikali ya rais wa Kenya William Ruto, Jumanne, imewatangaza wabunge saba wa Kenya Kwanza watakao shiriki katika mazungumzo na upinzani unaoongozwa Raila Odinga ili kumaliza uhasama wa kisiasa kati ya pande hizo mbili.

Hata hivyo chama hicho tawala kimesema hakitashiriki mazungumzo yoyote yatakayohusu kurejeshwa kazini kwa makamishna wanne wa IEBC waliofutwa kazi na Rais Ruto pamoja na kushiriki katika harakati za ufunguaji wa seva za uchaguzi.

Majadiliano hayo si ishara ya udhaifu wala njia ya kuishinikiza serikali kukubaliana na matakwa ya wapinzani wake.

Mazungumzo hayo yanayotarajiwa kufanyika katika mfumo wa bunge, yatahudhuriwa na wabunge wa chama tawala ambao ni pamoja na Boni Khalwale, Hillary Sigei, Adan Keynan, Lydia Haika, George Murugara, Essy Okenyuri na Mwengi Mutuse.

Mazungumzo hayo yatahusu hali ngumu ya maisha, ufufuaji wa uchumi na kuundwa kwa tume ya uchaguzi IEBC na kuwepo kwa makubaliano ya kisiasa.

Kiongozi wa Shughuli za Serikali katika bunge la taifa, Kimani Ichung’wa ameleeza.

Aidha muungano huo pia umepuuza madai ya Odinga kuwa alishinda kinyang'anyiro cha urais katika uchaguzi wa Agosti 9, 2022, na kusema kuwa Odinga anahitajika kuwasilisha madai yake mbele ya mahakama ya juu ili kufanya tathmini mpya ya maamuzi yaliyotolewa dhidi ya kesi aliyoiwasilisha ya kupinga ushindi wa rais Ruto, na kwamba msisitiza kuwa suala la kufungua seva za tume ya uchaguzi halifikiriwi kwa sasa.

Ichung’wa alisema upinzani umewasilisha mapendekezo saba katika mazungumzo kati yake na serikali ya Ruto ikiwa pamoja na hatua za haraka za kupunguza bei za unga, umeme na mafuta na ada za shule, na kutaka ukaguzi wa kitaalamu wa seva zinazotumiwa na IEBC kabla, wakati na baada ya uchaguzi wa urais 2022, mapitio ya uteuzi.

Na kuongeza kuwa upinzani pia umependekeza kufukuzwa kazi kwa Makamishna wa tume ya uchaguzi, ili kuimarisha na kuboresha mfumo uchaguzi ulio huru na wa haki

Kennedy Wandera, VOA Nairobi.

XS
SM
MD
LG