Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 23:41

EARDC yazishuku nchi jirani kuhusika na mgogoro wa DRC


Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) wakikabidhi bendera kwa rais wa nchi hiyo, William Ruto kabla ya kupelekwa DRC kama sehemu ya EARDC. Picha na Tony KARUMBA/AFP.
Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) wakikabidhi bendera kwa rais wa nchi hiyo, William Ruto kabla ya kupelekwa DRC kama sehemu ya EARDC. Picha na Tony KARUMBA/AFP.

Kikosi cha jeshi la kikanda kilichopelekwa eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ili kuleta amani kwenye eneo hilo lenye mzozo mkubwa kinazua mashaka kuhusu kuhusika kwa nchi jirani katika mzozo huo.

Dazeni ya makundi yenye silaha yamejaa huko mashariki mwa DRC, makundi ambayo ni muendelezo wa matokeo ya vita katika kanda hiyo ambavyo vilipamba moto katika miaka ya 1990 na 2000.

Kundi moja, la M23, limekuwa likifanya uharibifu tangu lilipoibuka tena mwishoni mwa mwaka 2021.

Rwanda imedaiwa kuliunga mkono kundi la waasi la M23, ambalo limeteka maeneo mengi katika jimbo la Kivu Kaskazini na kuwakosesha makazi maelfu ya watu.

Mwezi Juni mwaka jana nchi saba za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ziliamua kuunda kikosi cha kijeshi ili kukabiliana na mzozo huo.

Kenya walituma wanajeshi wake mwezi Novemba, wakifuatiwa na Burundi, Uganda na Sudan Kusini ambao wamepeleka vikosi vyao katika wiki za hivi karibuni.

Idadi ya kikosi hicho cha EAC haijulikani, lakini wanajeshi wako katika maeneo amgayo awali yalikuwa yakikaliwa na M23 na wana azma ya kusimamia kuondoka kwa waasi.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni alisema wiki iliyopita wanajeshi wake walikuwa "kikosi kisichoegemea upande wowote" na hakitapambana na M23.

Msururu wa wanajeshi wa kigeni, hususani wale wa Uganda, wanatiliwa mashaka katika baadhi ya maeneo ya DRC.

Denis Mukwege, daktari kutoka Congo ambaye alishinda Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2018 kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa ubakaji katika eneo hilo, hivi karibuni aliandika kupitia mtando wa Twitter kwamba jeshi la EAC limeundwa na "nchi zinazovuruga," kwa mfano.

Uganda ina historia ya kuingilia mzozo uliopo mashariki mwa Congo. Wengi pia wanashuku Uganda kuhusika katika mgogoro wa M23.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG