Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:37

Kainerugaba asema ananuia kugombea urais Uganda mwaka 2026


Jenerali Muhoozi Kainerugaba, mshauri maalum wa rais kwa operesheni maalum.
Jenerali Muhoozi Kainerugaba, mshauri maalum wa rais kwa operesheni maalum.

Mtoto wa kiongozi wa Uganda, Yoweri Museveni, amesema ananuia kugombea urais mwaka 2026, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Jenerali huyo kutoa muda wa  kuchukua nafasi ya baba yake ambaye ameiongoza nchi hiyo ya Afrika Mashariki kwa miaka 37.

Upinzani nchini Uganda kwa muda mrefu umekuwa ukimshutumu Museveni kwa kutaka kusimika utawala wa kifalme nchini Uganda na kudai kuwa alikuwa akimtayarisha mwanawe Muhoozi Kainerugaba kuchukua nafasi yake. Museveni amekanusha tuhuma hizo.

Hivi sasa akiwa ni mshauri maalum wa rais kwa operesheni maalum, Jenerali huyo mwenye umri wa miaka 48 anajulikana kwa kurusha ujumbe wa kutatanisha ambao umemfanya akaripiwe mara kadhaa na baba yake.

Kainerugaba alifuta haraka ujumbe kuhusu nia yake ya kuwnaia urais ambayo alikuwa amechapisha kwenye mtandao waTwitter siku ya Jumatano.

"Siku zote mmetaka niseme sawa, kwa jina la Yesu Kristo Mungu wangu, kwa jina la vijana wote wa Uganda na ulimwengu na kwa jina la mapinduzi yetu makuu nitasimama kugombea Urais mwaka 2026," Kainerugaba aliandika.

Katika tweet nyingine, alionyesha kutokuwa na subira kwa kusubiri kwa muda mrefu kuchukua nafasi ya baba yake.

"Waziri Mkuu wa Uingereza ana umri wa miaka 42, Waziri Mkuu wa Finland ana miaka 37. Baadhi yetu tunakaribia miaka 50. Tumechoka kusubiri milele," alisema.

Awali Kainerugaba aliwahi kuwa kamanda wa majeshi ya nchi kavu lakini aliondolewa katika nafasi hiyo baada ya kutishia kuivamia nchi jirani ya Kenya, jambo ambalo baadaye alisema ni mzaha.

XS
SM
MD
LG