Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 03:03

Upinzani nchini Kenya waandaa mikutano ya hadhara kwa kusubiri mazungumzo na serikali


Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga

Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya Jumanne ulitangaza mipango kwa ajili ya mkutano wa hadhara lakini ukasema bado una dhamira ya kupunguza mvutano wa kisiasa kupitia mazungumzo, baada ya maandamano ya kuipinga serikali kugeuka ghasia mwezi uliopita

Azimio la Umoja, muungano unaoongozwa na mwansiasa mkongwe wa upinzani Raila Odinga ulisema “utafanya mazungumzo ya moja kwa moja” na umma ikiwemo mkutano mjini Nairobi, unapojiandaa kwa mazungumzo na serikali.

Mwezi uliopita, watu watatu walifariki na biashara na mali zikachomwa moto na kuporwa katika siku tatu za maandamano mabaya ya kuipinga serikali.

Odinga, ambaye anadai aliibiwa uchaguzi wa rais wa mwaka uliopita, alisitisha maandamano baada ya Rais William Ruto kupendekeza wafanye mazungumzo kujadili hoja zao.

Muungano huo wa Azimio umesema utafanya mkutano wa ndani ya ukumbi Alhamisi ukifuatiwa na mkutano wa hadhara Jumapili “ili kuwaelezea watu wapi tulipo na hatua inayokuja.”

XS
SM
MD
LG