Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:14

Wafuasi wa Odinga wafutiwa mashtaka


Mabomu ya kutoa machozi yakiwa yamelipuliwa kila mahali wakati wa mkutano ulioitishwa na Raila Odinga jijini Nairobi, Machi 27, 2023. Picha na Yasuyoshi CHIBA / AFP.
Mabomu ya kutoa machozi yakiwa yamelipuliwa kila mahali wakati wa mkutano ulioitishwa na Raila Odinga jijini Nairobi, Machi 27, 2023. Picha na Yasuyoshi CHIBA / AFP.

Mwendesha mashtaka mkuu nchini Kenya Jumatatu alifuta mashtaka kwa wabunge wanne walioshiriki maandamano ya kuipinga serikali, hatua hii imekuja siku moja baada ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga kusitisha maandamano hayo, wakili wao alisema.

Odinga alisema Jumapili kuwa yuko tayari kwa mazungumzo na Rais William Ruto, endapo mamlaka itasitisha ukamataji kwa wale wanaohusishwa na maandamano, na kushughulikia suala la kupanda kwa gharama ya maisha na mageuzi ya mfumo wa uchaguzi.

"Kesi imefutwa ... kwa ajili ya amani, mazungumzo na haki kati ya watuhumiwa na serikali," wakili Danstan Omari aliliambia shirika la habari la Reuters.

Maelfu ya watu walishiriki maandamano mara tatu katika kipindi cha zaidi ya wiki mbili zilizopita wakipinga kupanda kwa bei za bidhaa na madai ya udanganyifu wa kura wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana.

Mara zote tatu, maandamano yaligeuka ghasia, maandamano mengine ya mara ya nne yalipangwa kufanyika Jumatatu.

Wabunge hao wanne wa upinzani wakiwemo viongozi wa kundi la Odinga katika mabunge yote mawili, walikamatwa na kufungiliwa mashtakiwa kwa kushiriki katika mkusanyiko kinyume cha sheria mwishoni mwa mwezi Machi, na baadaye waliachiwa kwa dhamana.

Kupitia mtandao wa Twitter, Ruto alisema amewaomba viongozi wa mabunge yote mawili kutoa kipaumbele katika kushughulikia maswala yote yaliyoibuliwa na upinzani.

"Tuna imani kuwa masuala yatashighulikia kikamilifu na bunge ili kuturuhusu kulenga katika progamu za mageuzi ya uchumi” aliongeza rais Ruto.

Ubalozi wa Marekani nchini Kenya na Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali ya kieneo (IGAD) waliungana na viongozi wa Kenya ili kukaribisha hatua ya mazungumzo.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG