Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:12

Polisi ya Kenya yapiga marufuku maandamano


Mkuu wa polisi wa Kenya ametangaza kupiga marufuku maandamano mapya ya upinzani yaliyoitishwa Jumatatu, baada ya maandamano ya wiki iliyopita kugeuka  ghasia.

Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome aliwaambia wanahabari Jumapili kamba hawata ruhusu maandamano yenye vurugu.

Amesema maandamano ya kesho ni kinyume cha sheria na hayataruhusiwa, na kuongeza kuwa jeshi lake liko tayari kulinda amani huku wakimkamata yeyote atakayebeba silaha za kivita.

Lakini mwanasiasa mkongwe wa upinzani Raila Odinga, ambaye ametoa wito kwa watu kujitokeza barabarani Jumatatu na Alhamisi kumpinga Rais William Ruto, kushindwa kukabiliana na gharama ya juu ya maisha, anaendelea kukaidi.

Katika ibada ya Jumapili, Odinga amewaomba wafuasi wao na Wakenya wote kujitokeza kuandamana kwa amani.

“Nataka kumwambia Bw Ruto na IG Koome kwamba hatutatishika,” amesema.

Maandamano ya Jumatatu iliyopita ambayo pia hayakuidhinishwa na polisi yalizusha ghasia, huku polisi wa kutuliza fujo wakiwarushia gesi ya machozi na maji ya kuwasha watu waliokuwa wakirusha mawe na kuchoma matairi.

Mwanafunzi wa chuo kikuu aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi huku maafisa 31 wakijeruhiwa katika mapigano jijini Nairobi na ngome za upinzani magharibi mwa Kenya, kulingana na polisi.

Zaidi ya watu 200 walikamatwa, wakiwemo wanasiasa kadhaa wakuu wa upinzani, huku msafara wa Odinga mwenyewe ukipigwa na mabomu ya machozi na maji ya kuwasha.

XS
SM
MD
LG