Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 19:04

Wavamizi wa shamba la rais wa zamani wa Kenya watachukuliwa hatua


Mfuasi wa upinzani akiwa ameshika jiwe wakati akikabiliana na polisi huko Mathare , Nairobi Machi 27, 2023. Picha na Luis Tato / AFP.
Mfuasi wa upinzani akiwa ameshika jiwe wakati akikabiliana na polisi huko Mathare , Nairobi Machi 27, 2023. Picha na Luis Tato / AFP.

Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano nchini Kenya, NCIC, Jumanne, imelaani uvamizi wa ya mali ya watu binafsi uliofanywa na wavamizi dhidi ya shamba kubwa linalomilikiwa na familia ya aliyekuwa rais nchi hiyo Uhuru Kenyatta.

Shamba hilo lililoko katika kaunti ya Kiambu nje kidogo ya jiji la Nairobi, lilivamiwa na makundi hayo ambayo pia yaliripotiwa kupora mali yenye thamani isiyojulikana.

Shambulio kama hilo liliripotiwa lilifanyika pia katika kampuni ya kutengeneza mitungi ya gesi ya Specter East Africa, kampuni ambayo inamilikiwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga, ambaye anaongoza maandamano hayo dhidi ya serikali, yakidai haki katika uchaguzi mkuu uliofanyika mawaka jana pamoja na kupunguza gharama za juu ya maisha.

Uvamizi wa kampuni ya kutengeneza gesi ya Odinga ilikuwa kisingizio cha kutatua mgigoro ya zamani ya umiliki wa ardhi.

Mwenyekiti wa NCIC, Samuel Kobia, ametaja uharibifu huo wa mali kuwa hauna maana, na kusema vitendo si halali kusababisha matatizo zaidi.

NCIC inoanya matendo mengine ya uharibifu wa magari, misikiti, makanisa na mali za watu binafsi kuwa havikubaliki na kwama endapo hakuna hatua itakayochukuliwa vitendo kama hivi vitaendelea na kuvuruga amani na pia kuleta wasiwasi na kuendeleza mivutano ambayo itasababuisha mizozo ya kidini na kikabila.

Jumatatu, wakati wafuazi wa upinzani ulipokuwa wakiandamana kwenye mitaa ya maeleo ya Mabanda Kawangware na Kibra, makundi hayo madogo ya wahuni yalivamia mali za watu na kufanya uharibifu huo.

Imeripotiwa makundi hayo ya yalinaswa kwenye video zilizosambazwa mitandaoni huku yakiwa yamebeba wanyama kama vile kondoo na kuwapakia kwenye magari yao. Miongoini mwao wanaripotiwa kuuza wanyama hao kwa wapita njia wa eneo hilo.

Muda mfupi baadaye, makundi mengine ya watu yalinaswa kwenye video yakifanya uvamizi wa kampuni ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga inayosemekana kutengeneza mitungi ya gesi inayojulikana kama kama East Africa Specter International katika Eneo la Industrial Area, hatua chache kutoka jiji kuu la Nairobi.

XS
SM
MD
LG