Maandamano ya awali yaliyoitishwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga Jumatatu yakipinga kupanda kwa gharama za maisha na kudai udanganyifu wa kura wakati wa uchaguzi kuu aliofanyika mwaka jana, ambayo umezua visasi kutoka pande zote mbili zikishambuliana, kitendo ambacho kimewafanya viongozi katika jamii kuwasihi kuleta utulivu.
Maandamano ya Alhamisi mchana katika mji mkuu wa Nairobi yalikuwa na utulivu zaidi ikilinganishwa na maandamano yaliyofanyika siku mbili zilizopita, hata hivyo maandamano hayo yalionekana kupamba moto majira za mchana.
Huko Mathare, makazi ya watu wenye kipato cha chini yaliyoko Nairobi, waandamanaji walitumia manati ya kienyeji kuwarushia mawe polisi waliovaa mavazi maalumu ya kwa ajili ya mapambano, picha za video za televisheni nchini Kenya iliyoonyesha.
Odinga akiambatana na viongozi wengine wa upinzani, alipitia katika vitongoji vingine vingi vya Nairobi wakati mamia ya waandamanaji wakiwafuata, wakiwa wamenyanyua fimbo, sufuria na miko ya kupikia.
Maandamano hayo yalikuwa ya amani zaidi, ripota wa shirika la habari la Reuters ambaye alikuwa akifuatilia tukio hilo alisema, lakini walipokuwa wakipita katika kituo cha polisi baadhi ya waandamanaji walikirushia mawe na kuwafanya polisi tumumia mabomu ya kutoa machozi.
Siku ya Jumatatu, kanisa na msikiti iliyoko Nairobi, katika wilaya ya Kibera ambayo inayokaliwa na watu wenye kipato cha chini ilichomwa moto, wakati mali zilizokuwa zikimilikiwa na familia ya Odinga na aliyekuwa raisi ya nchi hiyo Uhuru Kenyatta, ambaye waliomuunga mkono Odinga katika uchaguzi huo, waliharibiwa.
Chanzo cha habari hii ni Shirka la habari la Reuters