Mapigano hayo yamesababisha wasiwasi wa kuongezeka kwa hali mbaya ya kibinadamu.
Makubaliano ya kusitisha vita, ambayo yanafuatiliwa na Saudi Arabia pamoja na Marekani, yalipatikana baada ya wiki tano za mapigano mjini Khartoum na sehemu nyingine za Sudan, ikiwemo katika eneo la Darfur ambalo limeshuhudia ukosefu wa amani kwa muda mrefu.
Mapigano ya Sudan yanahusu mgogoro wa madaraka kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha jeshi la dharura RSF.
Yamepelekea kuwepo hali mbaya ya kibinadamu, na zaidi ya watu milioni 1 laki 3 kuhama makwao, pamoja na kuyumbisha usalama wa eneo hilo lenye misukosuko.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema kwamba kuna ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha vita, ikiwemo matumizi ya ndege za kivita, silaha na ndege zisizokuwa na rubani.
Marekani imeonya kwamba kundi la mamluki wa Russia, Wagner, limekuwa likitoa silaha ikiwemo makombora ya anga, kwa kikosi cha RSF kupigana na jeshi la Sudan na kusababisha mapigano kuendelea.
Forum