Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:09

Mapigano Sudan yamepungua lakini bado hayajasitishwa kikamilifu


Mfano wa majengo ya makaazi yaliyoharibiwa kufuatia vita vinavyoendelea nchini Sudan
Mfano wa majengo ya makaazi yaliyoharibiwa kufuatia vita vinavyoendelea nchini Sudan

Washington na Riyadh ambao walisimamia makubaliano ya sitisho la mapigano kati ya vikosi vya majenerali wawili hasimu, hata hivyo walielezea kwenye ripoti wakiashiria pande zote mbili zilikiuka makubaliano

Mapigano yamepungua nchini Sudan lakini hayajasimama leo Jumatano, siku ya pili kamili ya usitishaji mapigano ambalo limeibua matumaini ya tahadhari miongoni mwa raia wanaohangaika ambapo njia za misaada na barabara zinazotumika kwa ajili ya kukimbia mapigano hayo zitafunguliwa hivi karibuni.

Mashambulizi ya anga na mashambulizi ya silaha bado yamesikika kote katika mji mkuu, wakaazi wameliambia shirika la habari la AFP, lakini waangalizi wa Marekani na Saudi Arabia wanasema mapigano mjini Khartoum yanaonekana kupungua tangu kuimarishwa kwa sitisho la mapigano la wiki moja siku ya Jumatatu jioni.

Washington na Riyadh ambao walisimamia makubaliano ya sitisho la mapigano kati ya vikosi vya majenerali wawili hasimu hata hivyo walielezea kwenye ripoti wakiashiria pande zote mbili zilikiuka makubaliano.

Hata hivyo wanasisitiza kuwa maandalizi yanaendelea kupeleka misaada ya kuokoa maisha kwa watu wa Sudan ambao wamevumilia zaidi ya wiki tano za mapigano ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,000.

Forum

XS
SM
MD
LG