Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:16

Juhudi za usitishaji mapigano Sudan zafifia


Moshi ukifuka juu ya majengo katika jiji la Khartoum tarehe 19, Mei 2023. Picha na shirika la habari la AFP.
Moshi ukifuka juu ya majengo katika jiji la Khartoum tarehe 19, Mei 2023. Picha na shirika la habari la AFP.

Milipuko iliutikisa tena mji mkuu wa Sudan siku ya Jumanne, na kufanya matumaini ya usitishaji mapigano kwa ajili ya kusambaza misaada ya kibinadamu unaosimamiwa na Marekani pamoja na Saudi Arabia kufifia, baada ya mapigano yanayoendelea kwa zaidi ya wiki tano

Makubaliano rasmi ya hivi punde ya wiki moja yalianza kutekelezwa Jumatatu jioni, lakini haraka yamekiukwa, kama msururu wa makubaliano yaliyopita tangu vita kati ya majenerali wawili hasimu vilipoanza Aprili 15.

"Tunaweza kusikia sauti ya milio ya risasi," shuhuda mjini Khartoum aliliambia shirka la habari la AFP siku ya Jumanne. "Kila dakika chache, kuna mlipuko."

Wakaazi wa Khartoum pia wameripoti mapigano kaskazini mwa Khartoum pamoja na mashambulio ya anga yanayofanyika eneo la mashariki mwa mji mkuu muda mfupi baada ya muda wa mwisho kufika, siku ya Jumatatu saa tatu usiku.

Kulingana na shirika la habari la Reuters, pia wakazi wa jiji la khartoum wameripoti milio ya makombora ikisikika katika eneo la Khartoum pamoja na ndge za kivita zikiruka angani leo Jumanne, wakaazi walisema , khofu imeongezeka na kwamba mapigano makali yanaweza kuvuruga matumaini makubwa ya wausdan kutoka na sitisho la mapigano ambalo linasimamiwa kimataifa.

Mapigano hayo yamewakutanisha jeshi, linaloongozwa na kiongozi mkuu wa Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, dhidi ya ikosi vya Msaada wa Haraka vya kijeshi vinavyoongozwa na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdan Dagalo.

Katika baadhi ya maeneo ya Khartoum kumezuka ukimya wa hali ya juu siku ya Jumanne huku wakaazi wa mji huo wakitarajia kusitishwa kwa mapigano ili kuruhusu misaada ya kibinadamu ya kuokoa maisha, au kuwawezesha watu wengi zaidi kuukimbia mji huo wenye watu million tano uliokumbwa na mzozo.

Mapigano hayo yamesababisha vifo vya watu takriban 1,000, na kuwalazimisha zaidi ya milioni moja kuyakimbia makazi yao na kusababisha uhamishaji mkubwa wa wageni na wakimbizi kwenda katika nchi jirani.

Chanzo cha habari za taarifa hii zinatoka shirika la habari la Reuters na AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG