Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 07:52

Uporaji wakithiri katika jiji la Khartoum


Wenyeji wamekusanyika baada ya kuwatimua waporaji waliovamia duka la kuuza magari huko Khartoum, tarehe 7 Mei 7, 2023. Picha na AFP.
Wenyeji wamekusanyika baada ya kuwatimua waporaji waliovamia duka la kuuza magari huko Khartoum, tarehe 7 Mei 7, 2023. Picha na AFP.

Uporaji uliokithiri unaofanywa na watu wenye silaha na raia unafanya maisha ya wakazi wa Kartoum waliokwama katika mapigano makali kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha Rapid Support Forces (RSF) yawe mabaya sana, mashuhuda walisema.

Wakati RSF imeukamata mji mkuu, jeshi linafanya mashambulizi ya anga ya mara kwa mara, mashuhuda walisema polisi wametoweka mitaani wakati mapigano yalipoanza Khartoum Aprili 15.

"Hakuna anayetulinda. Hakuna polisi. Hakuna serikali. Wahalifu wanavamia nyumba zetu na kuchukua kila kitu tunachomiliki," Sarah Abdelazim mwenye umri wa miaka 35, ambaye pia ni mfanyakazi wa serikali alisema.

Huku ghasia zikiwa zimeikumba Khartoum, jeshi linaituhumu RSF kwa uporaji kwenye mabenki, masoko ya dhahabu, nyumba na magari. RSF inakanusha madai hayo na imetoa video zinazoonyesha watu wake wakiwakamata waporaji. Jeshi hilo limesema baadhi ya watu huvaa sare za RSF na kuiba ili kuwafanya waonekane wabaya.

Baadhi ya mashuhuda walisema RSF ilikuwa ikiiba magari na kuweka kambi kwenye nyumba za watu. Hili pia limekanushwa na RSF.

Zaidi ya wanaume 17,000 ambao waliokuwa wamefungwa katika jela mbili hatari sana nchini Sudan -- Kobar na Al Huda -- waliachiliwa mara baada mapigano kuanza. Pande zote mbili zinalaumiana kwa kuifungia jela.

'Mji wa Ibilisi'

"Sasa tunaishi katika mji wa ibilisi. Watu wanapora kila kitu na hakuna cha jeshi, RSF wala polisi, hakuna hata mmoja wao anayetaka kuwalinda watu wa kawaida. serikali liko wapi?" alisema Mohamed Saleh mwenye umri wa miaka 39, ambaye pia ni mwalimu wa shule ya msingi.

Mapigano hayo yalizuka baada ya mivutano kuhusu mipango ya kikosi cha RSF kujiunga na jeshi na mlolongo wa mamlaka kama sehemu ya mpito wa kisiasa. Mapigano hayo yamesababisha takriban watu 200,000 kukimbilia nchi jirani wakati zaidi ya 700,000 kukoseshwa makazi ndani ya Sudan, na kusababisha mzozo wa kibinadamu ambao unatishia kuleta ukosefu wa uthabiti katika ukanda huo.

Mapigano makali yanaendelea kupamba moto mjini Khartoum na miji dada ya Bahri na Omdurman, licha ya mazungumzo yaliyosimamiwa na Saudi Arabia na Marekani kati ya jeshi na RSF yaliyofanyika mjini Jeddah yenye lengo la kusitisha mapigano na kuhakikisha huduma za kibinadamu zinafikiwa.

XS
SM
MD
LG