Saudi Arabia, ambayo imekuwa mwenyeji wa mazungumzo hayo yenye lengo la kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano, pia ilimwalika mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan kwenye mkutano wa Ijumaa wa Jumuiya ya Mataifa ya Kiarabu huko Jeddah, mwanadiplomasia huyo aliongeza.
Mzozo huo uliozuka ghafla mwezi mmoja uliopita umesababisha vifo vya mamia ya watu, kupelekea zaidi ya watu 200,000 kukimbilia katika nchi jirani, kuwakosesha makazi wengine 700,000 ndani ya nchi na hatari kwa mataifa ya nje kujihusisha na hivyo kuliyumbisha eneo hilo.
Licha ya kualikwa kwa Burhan kwenye mkutano wa Jeddah, hatarajiwi kuondoka Sudan kwa sababu za kiusalama, wanadiplomasia wengine wawili katika Ghuba walisema.
Burhan alialikwa kwa sababu yeye ni mkuu wa Baraza Kuu la Sudan ambalo lilikusudiwa kusimamia mpango wa mpito kuelekea utawala wa kiraia kabla ya mzozo kuzuka, mwanadiplomasia wa Saudi Arabia alisema. Mpinzani wake ambaye ni mkuu wa RSF Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana kama Hemedti, ndiye naibu mkuu wa baraza hilo.