Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:16

Sitisho jipya la mapigano Sudan laleta matumaini ya amani kwa raia


Wakazi wa Sudan.
Wakazi wa Sudan.

Watu wa Sudan wana matumaini kuwa kusitishwa mapigano kwa wiki moja  kupisha juhudi za kibinadamu kutamaliza madhila wanayopitia, saa chache kabla ya usitishaji mapigano kuanza kutekelezwa baada ya mfululizo wa matamko ya awali ya makabaliano kukiukwa.

Hata hivyo maafisa wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan wanasema mapigano hayo yanaweza kugeuka na kuwa mzozo wa kikabila endapo pande zinazozozana hazitaheshimu usitishaji mapigano ulio ongezwa. Idd Ligongo anasoma ripoti kamili.

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa, nchini Sudan, Volker Perthes, ameliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba kuongezeka kwa ukabila kunahatarisha kuongeza na kurefusha na athari kwa eneo hilo.

Amezungumza hayo saa chache kabla ya usitishaji mapigano wa wiki moja kuanza baina ya makundi mawili ya jeshi yanayopigana. Perthes amesema tayari kumetokea dalili mwezi uliopita wa mapigano kutishia kugawanya nchi kwa misingi ya kikabila na kijamii.

"Dalili za tahadhari za uhamasishaji wa kikabila pia zinaripotiwa katika maeneo mengine ya nchi, haswa katika mikoa ya Kordofan Kusini, na Blue Nile. Mapigano nchini kote yamesababisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na ukiukwaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu na kudhoofisha ulinzi wa raia,” alisema Perthes.

Baada ya kuanzisha usitishaji wa mapigano ulio thabiti, ameliambia baraza la usalama, kipaumbele namba mbili cha Umoja wa Mataifa ni kuzuia kuongezeka au kueneza ukabila katika mzozo.

Perthes alipendekeza usitishaji mapigano na ulikubalika Jumamosi kuanzia saa tatu na dakika 45 usiku Jumatatu, ikiwa ni maendeleo ya kukaribishaw licha ya mapigano kuendelea hadi Jumatatu.

Licha ya makubaliano yaliyovunjwa awali, raia waliochoshwa na vita wamebaki na matumaini kwamba usitishaji mapigano utaendelea ili kuruhusu usambazwaji wa misaada kama vile chakula, dawa na rasilimali nyingine muhimu. Adam Othman ana matumaini na maafikiano ya Jeddah.

“Makubaliano ya Jeddah ni mafanikio ya kweli kwa watu wa Sudan, yatapunguza mateso tunayopitia. Suluhu ya vita duniani kote huanza na mazungumzo na mapatano. Kwa hiyo tunatumaini kuwa mapatano haya yatakuwa na nafasi na yatatekelezwa ipasavyo,” alisema Othman.

Kwa wakazi kama Souad al-Fateh anayeishi katika jiji pacha la Omdurman katika mji mkuu wa Nile, ahadi za hivi karibuni za mapatano zinaweza kuwa njia ya kuokoa maisha.

Al-Fateh alkisema; “Tunataka makubaliano. Tunataka walio madarakani wakubaliane. Sote tuna njaa, watoto na wazee. Kila mtu anateseka na vita. Hatuna maji tena. Tuna njaa kweli kweli. Lazima wafikie makubaliano.”

Kwa sasa, watu milioni 25 -zaidi ya nusu ya watu wote -wanahitaji misaada ya kibinadamu, Umoja wa Mataifa umesema.

Makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo yangeanza kutekelezwa Jumatatu usiku ni sehemu muhimu ya makubaliano ya awali yaliyotiwa saini na pande zinazozozana Mei 12 huko Jeddah, kuheshimu kanuni za kibinadamu na kuruhusu misaada inayohitajika sana.

Lakini makubaliano ya Mei 12 yalikuwa tayari yamekiukwa, kulingana na Umoja wa Mataifa ambao uliripoti takriban mashambulizi 11 yakilenga majengo ya kiraia huko Khartoum, na mashambulizi manne mapya dhidi ya vituo vya afya tangu Mei 12.

XS
SM
MD
LG