Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:04

Marekani yaonya "wanaohujumu mkubaliano ya kusitisha mapigano" Sudan


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, anaonya kwamba wanaokiuka makubaliano ya usitishaji mapigano ya Sudan watawajibishwa kwani makubaliano ya hivi karibuni kati ya pande mbili zinazozozana yameshindwa kutekelezwa saa kadhaa baada ya kuanza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, anaonya kwamba wanaokiuka makubaliano ya usitishaji mapigano ya Sudan watawajibishwa kwani makubaliano ya hivi karibuni kati ya pande mbili zinazozozana yameshindwa kutekelezwa saa kadhaa baada ya kuanza.

Wawakilishi wa jeshi la Sudan na vikosi hasimu vya wanajeshi wa akiba walikuwa walikubaliana kusitisha mapigano kwa siku saba ili kuruhusu kuanzishwa tena kwa huduma muhimu na misaada ya kibinadamu.

Makubaliano mapya zaidi ya sasa ya kusitisha mapigano yaliyotiwa saini na pande mbili zinazopigana za Sudan yalitokana na juhudi za diplomasia, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, alisema Jumanne kupitia Twitter.

Ingawa aliungwa mkono na Marekani na Saudi Arabia, Blinken alisema ni juu ya pande zinazozozana kutekeleza mapatano hayo.

"Ikiwa usitishaji mapigano utakiukwa, tuta-tambua na tutawawajibisha wanaokiuka kupitia vikwazo vyetu na nyenzo zingine tulizo nazo," alisema Blinken.

Haya yanajiri baada ya wapatanishi wa pande hizo mbili kwa mara ya kwanza kukubaliana kuunda timu ya kufuatilia usitishaji mapigano.

Kukiwa na mapigano makali mwishoni mwa juma na Jumatatu, mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa Sudan, Volker Perthes, alisema pande zinazozozana tayari zimekiuka makubaliano hayo kwa kushindwa kuheshimu ahadi zao ya kutofuata maslahi ya kijeshi katika saa 48 kabla ya usitishaji mapigano.

Hassan Khannenje, mkurugenzi wa taasisi ya kimataifa ya pembe ya taaluma za Kimkakati nchini Kenya, anasema kimsingi hakuna upande wowote katika vita vya Sudan ambao una nia kwa sasa ya kusitisha mapigano.

Khanenje alisema: “Sababu ni mkwamo uliopo, hesabu ni kwamba kila upande unaweza kutumia kuongeza faida katika uwanja wa mapambano ili kuimarisha matakwa yao katika meza ya mazungumzo kwa siku za usoni. Sasa kwa kuzingatia hilo hakuna aliye na motisha ya kusitisha mapigano kabisa wakati huu.”

Aliiambia VOA kwamba ili usitishaji mapigano ufanikiwe, lazima kuwe na uwezekano wa utekelezaji wake na hana uhakika kuwa kuna njia ya kufuatilia kwa ufanisi hali hiyo.

Wakati huo huo, makundi ya misaada bado yanajitahidi kutoa msaada unaohitajika katika maeneo mengi ya nchi.

Mjini Geneina, na Darfur Magharibi, takriban watu 100,000 waliokimbia makazi yao bado wanakabiliwa na madhila ya ghasia hizo, Karl Schembri wa baraza la wakimbizi la Norway ameiambia VOA.

“Hali ya Geneina bado si shwari. Wenzetu wenyewe wamelazimika kukaa ndani au kukimbia. Imekuwa nje ya udhibiti kwa wiki yote iliyopita mpaka sasa,” alisema.

Schembri alisema anatumai usitishaji vita wa hivi sasa utakuwa na aina fulani ya athari ingawa anasema matarajio yake si makubwa.

Madaktari wasio na mipaka yaani MSF, wanasema hivi karibuni walifanya karibu upasuaji 250 ndani ya wiki moja. Wengi waliofika katika hospitali kusini mwa Khartoum walipata majeraha ya risasi au majeraha yanayohusiana na milipuko ya hivi karibuni.

Umoja wa Mataifa unasema tangu vita vilipoanza katikati ya mwezi wa Aprili, zaidi ya raia 860 wameuawa, karibu watu milioni moja wameyakimbia makazi yao na robo milioni wengine wamekimbilia nchi jirani.

Forum

XS
SM
MD
LG