Lakini sitisho la mapigano la wiki nzima, ni makubaliano ya hivi karibuni baada ya mfululizo wa makubaliano ya awali kukiukwa, na makubaliano ya sasa kukiukwa dakika chache tu baada ya kuanza kutekelezwa Jumatatu usiku.
Tangu wakati huo, makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo yalikusudia kuruhusu usambazaji wa misaada ya kibinadamu kwenye maeneo yanayoathiriwa zaidi kutokana vita hivyo, yalivunjwa mara kadhaa, huku pande zinazozana zikilaumiana.
Katika mji mkuu wa Darfur Kaskazini wa El Fasher, wakazi wameripoti mapigano kwa kutumia kila aina ya silaha, katika vita vya wiki sita kati ya jeshi la taifa linaloongozwa na Abdel Fattah al-Burhan, na kikosi cha Rapid Support Forces (RSF).
Mapigano hayo yaliyozuka tarehe 15 Aprili, yamewaua zaidi ya watu 1,800.
Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya Wasudan milioni moja wamelazimishwa kuhama makazi yao, huku watu wengine 300,000 wakikimbilia katika nchi jirani.
Forum