Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:22

Ukatili na wizi watawala Khartoum


Watu wakiwa sokoni huko kusini mwa Khartoum, tarehe 24 Mei 2023, baada ya usitishaji vita uliosimamiwa na Marekani na Saudia. Picha na AFP.
Watu wakiwa sokoni huko kusini mwa Khartoum, tarehe 24 Mei 2023, baada ya usitishaji vita uliosimamiwa na Marekani na Saudia. Picha na AFP.

Wakati mapigano mjini Khartoum yakiingia siku ya 22, raia waliobaki mjini humo walielezea hai mbaya ya kikatili. Wengi wakikaribia kuishiwa na mahitaji muhimu, masoko yakiwa yamefungwa na bidhaa kutoka nje haziingi tena nchini.

Yousif Ahmed mmiliki wa duka na mfanyabiashara mjini humo, alielezea hali hiyo mbaya. Amesema hali "si thabiti," watu wanalazimika "kuiba" ili tu kuishi. "Tunalazimika kuiba ili tupate riziki ya kujikimu kwa siku na siku zijazo, sasa kila kitu kimepotea, tunateseka sana kutokana na janga hili, watu wote inawalazimu kuiba kila wiki," aliiambia VOA.

Ahmed alisema ukosefu wa usalama mjini humo pia unamaanisha kuwa wafanyabiashara wanapaswa kubuni njia za kulinda bidhaa zao ili kuepuka kuibiwa.

“Kwangu mimi kama muuza mboga, hali ni mbaya sana. Hakuna bidhaa, tunahisi hakuna usalama kwa sababu tunaweza kuporwa wakati wowote. Baadhi ya wafanyabiashara wanahifadhi bidhaa majumbani mwao.”

Kulingana na Umoja wa Mataifa, takriban Wasudan milioni 19 wanaweza kuathiriwa na uhaba wa chakula kutokana na mzozo huo. Wanaharakati walisema dola milioni 445 zinahitajika ili kuwasaidia wakimbizi wanaoikimbia Sudan na kuwapatia misaada kwa kipindi cha miezi sita ijayo.

Mohammed Hassan Abu Shama, mkazi mwingine wa Khartoum alisema hali ya maisha katika jiji hilo inaendelea kuwa mbaya sana.

"Watu wameanza kuhifadhi chakula na maduka mengi hayana mahitaji ya msingi," aliiambia VOA. “Bei ya unga ni ghali sana, na bei ya mkate imepanda maradufu. Watu wanataka kusafiri nje ya Khartoum, lakini pia gharama ya tiketi iko juu, iwe ya majimbo au nje ya Sudan. Vita hivi viliharibu mambo mengi, tuna imani mambo yatakuwa mazuri.”

Lakini katika kipindi hiki cha ukofefu wa utulivu, na kukosekana kwa serikali inayofanya kazi na mashirika ya misaada, Wasudan waliopo katika baadhi ya vitongoji vya Khartoum waliweka mipango ya hiari kuwasaidia raia wenye kipato duni zaidi ili kuwapunguzia matatizo.

Hassan Mohammed Ahmed Salih kutoka kitongoji cha Jabra alielezea jinsi jamii inavyochukua hatua za kusaidia kuwalisha wale wenye shida.

"Tulipata kiasi cha unga kutoka kwa baadhi ya mawakala na kuwasambazia wananchi wengi maskini katika eneo hilo na kutatua tatizo la uhaba wa unga," alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG