Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:47

Vikosi vya ADF vyadaiwa kuuwa watu 26 Mashariki mwa DRC


Wanajeshi wa Congo wakifanya doria katika kijiji cha Mwenda kilichoko Kaskazini Mashariki mwa DRC Mei 23, 2021. Picha na ALEXIS HUGUET / AFP.
Wanajeshi wa Congo wakifanya doria katika kijiji cha Mwenda kilichoko Kaskazini Mashariki mwa DRC Mei 23, 2021. Picha na ALEXIS HUGUET / AFP.

Washukiwa wanamgambo wa Kiislamu waliwauwa takriban watu 26 katika shambulio lililotokea Oicha, mji ulioko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatatu usiku, meya wa mji huo Nicola Kikuku alisema siku ya Jumanne.

Aliyataja mauaji hayo kuwa yamefanywa na Allied Democratic Forces (ADF), kundi la wapiganaji la Uganda lenye makao yake mashariki mwa Congo ambalo limeahidi kulitii kundi la Islamic State na limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara.

Shambulio hilo lilitokea majira ya saa tano usiku, alisema meya wa Oicha katika jimbo la Kivu Kaskazini. Watu wanne walijeruhiwa na kupelekwa hospitali, alisema

Watu wanne walijeruhiwa na kupelekwa hospitali, alisema.

"Inasikitisha kwa sababu wakati huu kulikuwa hakuna onyo," alisema mwanaharakati wa jumuiya ya kiraia katika eneo hilo, Janvier Kasereka Kasayirio, ambaye alithibitisha shambulio hilo na pia kuilaumu ADF.

"Tumeweka miili 26 kwenye chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali kuu ya Oicha," alisema Darius Syaira, mwakilishi wa jumuiya ya kiraia katika eneo la Beni.

Alisema waliouawa ni watoto 12 na watu wazima 14, wengi wao waliuawa kwa visu.

Jeshi la Uganda lilisema mwezi uliopita lilifanikiwa kuwaua zaidi ya wapiganaji 560 na kuharibu baadhi ya kambi zao.

Uganda na DRC zilianzisha mashambulizi ya pamoja mwaka 2021 dhidi ya ADF ili kuwafukuza wanamgambo hao kutoka ngome zilizopo Congo, lakini mashambulizi yameendelea.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG