Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:15

Africa Kusini yaamuru wanajeshi wanaoshutumiwa kwa 'unyanyasaji wa kingono' DRC warudi nyumbani


Maafisa wa kijeshi chini ya ujumbe wa Monusco. Picha na Austere Malivika.
Maafisa wa kijeshi chini ya ujumbe wa Monusco. Picha na Austere Malivika.

Jeshi la Afrika Kusini lilisema Jumapili kuwa limewaamuru kurudi nyumbani wanajeshi wanane wanaotuhumiwa kwa utovu wa nidhamu unaohusiana na unyanyasaji wa kingono katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hadi uchunguzi ufanyike.

Wanane hao, sehemu ya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa (Monusco), walizuiliwa kwenye kambi zao katika mji wa mashariki wa Beni mapema mwezi huu.

"Kutokana na uzito wa madai hayo, SANDF ilichukua uamuzi wa kuwarejesha nchini Afrika Kusini wanajeshi waliohusika ili kujibu tuhuma hizo na kutoa maelezo ya matukio yaliyojiri," Jeshi la Ulinzi la Taifa la Afrika Kusini (SANDF) lilisema. Wachunguzi wametumwa DRC kufanya uchunguzi rasmi, taarifa hiyo iliongeza.

Wanajeshi hao wanaweza kuwa walihusika katika kile ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) ulikiita katika ripoti za ndani kama "ukiukaji mkubwa wa utaratibu" wa sheria za Umoja wa Mataifa.

Mapema wiki hii, msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric alisema MONUSCO ilipokea ripoti kwamba wafanyakazi waliohusika "walikuwa wakishirikiana, baada ya saa za amri ya kutotoka nje, katika baa ya nje ya mipaka inayojulikana kuwa mahali ambapo ngono inafanyika".

Tangu mwezi Mei, Rais wa Kongo Felix Tshisekedi amekuwa akitoa wito kwa nchi za SADC (Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika), ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini, kupeleka maafisa nchini mwake kuunga mkono jeshi la Kongo kukabiliana na waasi wa M23, ambao wameteka maeneo makubwa ya Jimbo la Kivu Kaskazini.

Kinshasa pia imekuwa ikitoa wito wa "kuharakishwa" kuondoka kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa kuanzia mwezi Disemba, ikikishutumu kwa kushindwa kukomesha ghasia za makundi yenye silaha kwa miaka 25 ya uwepo wake nchini humo.

Forum

XS
SM
MD
LG