Waasi wa M23 na wanamgambo watiifu kwa serikali ya Congo wamekuwa wakipambana kwenye eneo hilo katika siku za karibuni kinyume na makubaliano tete ya sitisho la mapigano ambalo lilidumu kwa miezi kadhaa.
Katika ushindi nadra dhidi ya M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, wanamgambo watiifu mwezi huu wameukomboa mji wa kimkakati wa Kitshanga kwenye jimbo la Masisi, Kivu Kaskazini.
Shirika la habari la AFP mwishoni mwa wiki lilitembelea eneo hilo ikiwa sehemu ya ziara iliyopangwa na jeshi la Congo, wakati maafisa wakisema kwamba jeshi linahakikisha makubaliano ya sitisho la mapigano na M23 yanaheshimiwa.
Lakini wakazi wengi wa mji huo na maafisa wa usalama wamese kwamba jeshi linawasaidia wanamgambo watiifu kwa serikali ambao wanajulikana kama Wazalendo.
Forum