Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 20:55

Uzalishaji chakula ni suluhisho kwa ukosefu wa ajira kwa vijana - Ripoti


Kiwango cha watu wasiokuwa na ajira wanaopata posho ya kujikimu duniani.
Kiwango cha watu wasiokuwa na ajira wanaopata posho ya kujikimu duniani.

Watalaamu katika kilimo, uhandisi, teknolojia, lishe na usalama wa chakula wamezindua ripoti ya kurasa 140 nchini Uganda wiki hii, wakiangalia changamoto zinazowakabili vijana wa kiafrika na elimu na ujuzi unaohitajika kwa ajili ya ajira katika sekta ya agrifood.

Rhoda Tumusiime, kamishna wa zamani kwa uchumi wa vjijini na kilimo katika Umoja wa Afrika, ni mmoja wa watalaamu, anasema biashara ya chakula inaweza kuboresha maisha ya vijana wa Kiafrika.

Tumusiime anaeleza: “Biashara ya chakula inatoa fursa kwa vijana kupata nafasi za ajira kwao wenyewe katika biashara ya kilimo na kuboresha maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Uwekezaji katika baishara ya usindikaji wa mazao ya kilimo na nguvu ya kuunganisha viungo vya mbele kwa masoko na biashara na viungo vya nyuma katika uzalishaji vinavyosababisha minyororo hii ya thamani ambayo itakuwa ni sekta ya msingi katika kuzalisha nafasi za ajira katika mifumo ya mazao ya kilimo."

Ripoti inatoa mifano. Nchini Zambia, mamlaka ilizindua YAPASA, mradi wa kuongeza mapato kwa vijana wa vijijini.

Mradi ulioko katika nchi ya Afrika ya Kati unahamasisha ushirikiano kati ya wahusika tofauti katika sekta ya kilimo – hasa wakulima wadogo – na kuwa na mawasiliano mazuri kati ya wazalishaji wadogo na wafanyabiashara wakubwa wa kilimo.

Kuratibu na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, Shirika la Kimataifa la Kazi – ILO, na serikali ya Zambia, YAPASA ilifungua nafasi 3,000 za ajira na kuboresha ujasiriamali wa vijijini unaoongozwa na vijana.

Benki ya Dunia inasema ukichanganya masoko na chakula na vinywaji inatabiriwa kuwa na thamani ya dola trilioni moja ifikapo mwaka 2030.

Ousmane Badiane ni mwenyekiti mwenza wa jopo ambalo limetoa ripoti. Ameiambia VOA ni muhimu kutengeneza sera kwa ajili ya vijana ili kuboresha mazingira ya biashara.

Badiane anafafanua: “Kuzifanya sera kuwa nyeti zaidi kwa mahitaji na utashi wa vijana utakuwa ni muhimu. Kufungua nafasi kwa kujihusisha na vijana itakuwa ni kitu muhimu sana kukifanya. Kuendeleza yote hayo katika miongo kadhaa ijayo kutahitaji kuwa na uwezo wa kuhimili ukuaji katika muktadha wa mabadiliko ya hali ya hewa, siyo tu katika kukabiliana na kuwa na ustahmilivu lakini pia kuwa na uwezo wa kubuni njia mpya za kufanya biashara.

kwa mujibu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, vijana milioni 11 wanaingia katika soko kutafuta ajira kila mwaka, lakini ni kiasi cha ajira milioni tatu rasmi zinatengenezwa kila mwaka. Barani Afrika, watu milioni 120 kati ya umri wa miaka 15 na 35 hawana ajira.

Mhadhiri wa uhandisi katika chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda, Dorothy Okello ameiambia VOA kuna haja ya kuunganisha fursa katika nyanja ya kilimo na elimu ya wanafunzi.

Okello anaelezea: “Tunaweza, kwa mfano, Uberization, kama naweza kutumia neno, la huduma za trekta? Kwahiyo, unajua, huduma kama trekata ambayo ina kila kitu, ambako kuna trekta moja inapatikana kwa wakulima kadhaa. Kwahiyo, tunakuwa vipi wabunifu katika kutumia uhandisi ili kuja na masuluhisho kwa hilo? Kama nikiwaangalia watu ambao wana ubunifu, Sanaa au Sanaa ya kiviwanda. Kwahiyo mwisho wa siku, ninapokuwa na bidhaa zangu na nataka kuziuza, nifanye nini ili kuzifanya zivutie kwenye soko?”

Watalaamu wanazitaka serikali za kiafrika kuwawezesha vijana kwa kuzungumzia vikwazo vya biashara, kuwekeza katika teknolojia, na kuwahusisha vijana katika kuandaa sera na kufanya maamuzi.

Ripoti ya mwandishi wa VOA Mohammed Yusufu

Forum

XS
SM
MD
LG