Ukusanyaji maoni mpya unaonyesha kwamba baadhi ya Wamarekani wana wasiwasi jinsi Rais Joe Biden anavyoshughulikia uchumi, licha ya serikali kutangaza mara kwa mara, takwimu chanya za kiuchumi.
Utafiti huo, pia unaonyesha kwamba, kufikia mwishoni mwa mwezi Januari, umaarufu wa Biden, ulikuwa asili mia 38, na unabashiri mapambano makali kati ya rais huyo, na mpinzani wake mkuu, Donald Trump, kuelekea kwa uchaguzi wa mwezi Novemba.
Utawala wa Biden unasema, uchumi wa Marekani umeimarika.
Kamala Harris, Makamu wa Rais wa Marekani anasema: "Katika kipindi cha zaidi ya miaka mitatu iliyopita, Rais Biden na mimi tumepunguza gharama, tumebuni fursa, na tumejenga uchumi unaowasaidia watu wanaofanya kazi. Tumebuni zaidi ya nafasi mpya milioni 14.5, za ajira, kuongeza mishahara kwa mamilioni ya Wamarekani. Imani ya wanunuzi imeongezeka na matumizi yako katika kiwango cha juu sana. ingawa tuna kazi zaidi ya kufanya, tuseme wazi: Uchumi wa Marekani unaendelea kuwa wenye nguvu zaidi duniani."
Mkuu wa benki kuu ya Marekani - ambayo inadumisha kwa dhati uhuru wake kutoka kwa shinikizo la kisiasa - anakubali.
Jerome Powell, Mwenyekiti wa Benki Kuu ya Marekani alieleza: "Tunahisi mfumuko wa bei unashuka. Ukuaji umekuwa wenye nguvu. Soko la ajira limekua. Tunachojaribu kufanya ni kufika mahali ambapo tunajiamini zaidi kuhusu mfumuko wa bei, na kuurejesha hadi asili mia mbili ili tuweze kuanza mchakato wa kuondoa kizuizi."
Lakini utafiti mpya wa maoni kutoka kwa kampuni ya utafiti ya Ipsos inaonyesha kuwa idadi inayoongezeka ya wapiga kura wa Marekani hawaamini hayo- na hiyo inaumiza nafasi za Biden za kuchaguliwa tena.
Cliff Young, Ipsos anasema: "Biden anaanza mwaka 2024 katika hali dhaifu. Utafiti wa maoni unauweka umaarufu waka katika asili mia 38. Na hiyo ni muhimu kwa sababu kulingana na uzoefu wetu, uzoefu wa kihistoria, rais aliye mamlakani, aliye na umaarufu wa asili mia 40, au bora zaidi, kulingana na utafiti wa maoni, ana nafasi bora zaidi ya 50-50 ya kushinda uchaguzi ujao.
Suala kuu la wapiga kura, Young anasema, ni uchumi, na siyo masuala makubwa zaidi.
Wapiga kura wa chama cha Democratic katika jimbo la South Carolina walimuunga mkono Biden kwa kiasi kikubwa katika uchaguzi wa mchujo wa hivi karibuni - lakini hata wafuasi wanasema gharama ya maisha iko juu.
Saundra Trower, Mpiga kura, South Carolina anaeleza: "Bidhaa zimepanda bei zaidi. Mafuta ya gari pia. Lakini kinachotia moyo ni kwamba viwango vya riba vya mikopo vinaanza kushuka."
Huo, Young anasema, ni mwelekeo mpya kutoka kwa msemo wa kisiasa wa enzi ya Clinton kwamba wapiga kura wa Marekani wanajali kipaumbele kimoja: "Uchumi."
Ripoti ya mwandishi wa VOA Anita Powell
Forum