Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 19:44

Idadi ya watu wasiokuwa na ajira imeongezeka Nigeria


Wafanyakazi wa kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo katika kijiji cha Obajana Nigeria
Wafanyakazi wa kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo katika kijiji cha Obajana Nigeria

Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Nigeria kimefikia asilimia 4.2 katika kipindi cha kati ya mwezi April mpaka Juni, kukiwa na mabadiliko kidogo kutoka mwaka jana, yakionyesha mwenendo mchanganyiko wa viashiria chanya na changamoto zilizopo.

Ukosefu wa ajira katika kipindi cha robo ya pili umeongezeka kidogo kutoka asilimia 4.1 katika robo ya kwanza ya mwaka, kulinga na data zilizochapishwa na Idara ya Taifa ya Takwinu.

Idadi ya vijana wasiokuwa na ajira kati ya umri wa miaka 15 mpaka 24 imeongezeka na kufikia asilimia 7.2 kutoka 6.9. Kiwango cha ukosefu wa ajira katika maeneo ya mijini pia kimeongezeka kufikia asilimia 5.9 kutoka asilimia 5.4.

Kiwango kikubwa cha watu wasio na ajira kimelikumba taifa hilo la Afrika lenye watu wengi na lililokuwa na uchumi mkubwa katika kipindi cha miongo kadhaa wakati idadi ya watu ikiendelea kuongezeka kwa kasi na kuushinda ukuaji wa uchumi wa taifa hilo lenye miundombinu duni, inayozuia usambazaji wa utajiri.

Watu wengi, takribani asilimia 88 wamejiajiri katika kipindi hicho cha kati ya mwezi April mpaka Juni, wakati asilimia 12 tu wana ajira za kulipwa mishahara.

Kiwango cha ukosefu wa ajira miongoni mwa waliomaliza elimu ya sekondari kimebakia katika asilimia nane, wakati kiwango cha ajira zisizo rasmi, kinachopima kiwango cha wafanyakazi wanafanyakazi katika maeneo ya uchumi yasiyo rasmi kubadilika kigogo kwa asilimia 92.7.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG