Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 18:57

Washambuliaji waua wanajeshi wanne na kuteka nyara raia wawili wa Korea nchini Nigeria


Ramani ya jimbo la Nigeria la Rivers
Ramani ya jimbo la Nigeria la Rivers

Watu wenye silaha walifanya shambulio la kuvizia dhidi ya msafara wa magari Kusini mwa Nigeria na kuua wanajeshi wanne, madereva wawili na kuteka nyara wafanyakazi wawili raia wa Korea, polisi wamesema Jumatano.

Utekaji nyara kwa ajili ya kupata fidia ni jambo la kawaida nchini Nigeria, na wafanyakazi wa kigeni wamekuwa wakilengwa na magenge ya wahalifu miaka iliyopita, hasa wale wanaofanya kazi katika maeneo ya mbali ya uchimbaji madini na miradi ya ujenzi.

Tukio hilo la hivi karibuni lilitokea mapema Jumanne kwenye barabara ya Ahoada/Abua kusini mwa jimbo la Rivers, polisi wamesema.

Afisa mkuu wa polisi katika jimbo hilo ameliambia shirika la habari la AFP” Washambuliaji walivizia msafara wa magari yaliyokuwa yakisafirisha wafanyakazi wawili wa kampuni ya Daewoo nyakati za saa tatu na nusu asubuhi. Wanajeshi wawili waliokuwa wanawashindikiza Wakorea na madereva wao wawili waliuawa katika shambulio hilo.”

Ameongeza kuwa bunduki za wanajeshi hao zilichukuliwa na washambuliaji hao.

Afisa huyo wa polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe ameongeza kuwa “ Washambuliaji waliwateka pia nyara Wakorea wawili kabla ya kutoroka.”

Forum

XS
SM
MD
LG