Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 21:40

Kiwanda cha Dangote Nigeria kimepokea mapipa milioni moja ya mafuta ghafi


Rais wa zamani wa Nigeria Muhammadu Buhari (katikati) akizindua kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote May 22, 2023. Picha na PIUS UTOMI EKPEI / AFP.
Rais wa zamani wa Nigeria Muhammadu Buhari (katikati) akizindua kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote May 22, 2023. Picha na PIUS UTOMI EKPEI / AFP.

Kiwanda kipya cha kusafisha mafuta Nigeria cha Dangote chenye thamani ya dola bilioni 19 kimepokea mapipa milioni moja ya mafuta kutoka kampuni ya Shell InternationalTrading and Shipping.

Hii ni shehena ya pili ya mafuta ghafi kwa mwezi huu, wakati kampuni hiyo ikijiandaa kuanza uzalishaji, msemaji wa kampuni alisema siku ya Jumatano.

Kiwanda cha kusafisha mafuta kiko nyuma kwa miaka mingi, lakini shughuli zake zinatarajiwa kuigeuza nchi hiyo ambayo ni mzalishaji mkubwa sana wa mafuta barani Afrika kuwa muuzaji mkubwa wa mafuta nje ya nchi.

Masemaji wa Dangote alikataa kusema mahali yanapotoka mafuta ghafi, lakini amesema shehena hiyo itaondolewa katika kiwanda cha kusafishia mafuta kilichopo nje ya Lagos siku ya Jumatano.

Dangote imesema, kiwanda kinatarajia shehena zaidi kusambazwa na kampuni ya taifa ya mafuta ya NNPC Ltd mwezi huu na shehena nyingine kutoka ExxonMobil.

Kiwango cha uzalishaji mafuta cha OPEC kwa Nigeria kwa mwaka ujao ni mapipa milioni 1.5 kwa siku, lakini serikali ina mpango wa kuzalisha mapipa milioni 1.8 kwa siku kuhakikisha inasambaza kwenye kiwanda cha Dangote na kwa viwanda vinavyomilikiw ana serikali ambavyo vimefanyiwa maboresho.

Chanzo Cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG