Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 02:22

Mahakama ya ECOWAS yatupilia mbali kesi ya utawala wa kijeshi Niger kutaka ifutiwe vikwazo


Wakuu wa Kamati ya ECOWAS walizungumza na waandishi wa habari hiko Ghana Agosti 18. 2023
Wakuu wa Kamati ya ECOWAS walizungumza na waandishi wa habari hiko Ghana Agosti 18. 2023

Mahakama ya Afrika Magharibi siku ya Alhamisi imetupilia mbali kesi ya utawala wa kijeshi iliyokuwa ikiomba kuondolewa kwa vikwazo vilivyowekwa na jumuiya hiyo kikanda ya ECOWAS kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika mwezi Julai.

Wanajeshi kutoka kikosi cha ulinzi wa rais wa Niger walimtia ndani Rais Mohamed Bazoum Julai 26 na kuunda kile walichokiita serikali ya mpito.

Serikali hiyo ya mpito iliiambia mahakama ya ECOWAS yenye makao yake Abuja kuwa, vikwazo hivyo ambavyo vinajumuisha kufungwa kwa mipaka kulikofanywa na majirani ya Niger na kukata usambazaji wa umeme haztua iliyochukuliwa na Nigeria kumepeleka uhaba wa dawa na chakula na kusababisha ugumu wa maisha.

Lakini mahakama ilitupilia mbali kesi hiyo na kusema kuwa utawala wa kijeshi haustahili kuwasilisha kesi kwa niaba ya Niger.

“Utawala wa kijeshi hautambuliki kama serikali na si mwanachama wa ECOWAS na kwa hiyo haiwezi kusughulikia suala lao. Kesi hii imefutwa” hakimu Dupe Atoki alitoa maamuzi.

Serikali hiyo iliyoundwa na jeshi ilisema mwezi Oktoba kuwa imepunguza mpango wake wa matumizi kwa mwaka 2023 kwa asilimia 40 kwa sababu ya vikwazo vilivyowekwa baada ya jeshi kunyakua madaraka, baada ya uchumi mbaya na ni moja ya taifa maskini sana duniani.

Nigeria ilikuwa na mshirika muhimu kwa nchi za Magharibi, ikiwemo Marekani katika mapambano dhidi ya wanamgambo wa kiislamu ambao wameua maelfu ya watu na kusababisha zaidi ya mamilioni ya watu kupoteza makazi.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG