Kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta cha Nigeria kilichojengwa na tajiri mkubwa zaidi barani Afrika Aliko Dangote, kilipokea bidhaa zake za kwanza za mafuta ghafi, kampuni hiyo imesema Jumamosi, katika hatua ya hivi karibuni ya kuanzisha mradi wa mkubwa sana uliochelewa.
Ikichukuliwa kama kiwanda kikubwa sana cha aina yake barani Afrika, kitasafisha mapipa 650,000 ya mafuta kwa siku, kiwanda cha Dangote kinaweza kuleta mabadiliko ya uchumi kwa Nigeria wakati kinafanya kazi kikamilifu ili kusaidia kumaliza utegemezi wa nchi hiyo kuagiza mafuta kutoka nje.
Kampuni ya Dangote Petroleum Refinery ilipokea shehena ya awali ya mapipa milioni moja ya mafuta ghafi, kutoka eneo la maji ya kina kirefu la Agbami, na ilianza kupakia bidhaa siku ya Ijumaa, msemaji wa kampuni hiyo alisema leo Jumamosi.
Hatua za awali zitakuwa kwa ajili ya uzalishaji wa dizeli na mafuta ya ndege kabla ya kuendelea na juhudi za uzalishaji petroli. Dangote hakutoa tarehe ya kuanza kwa uzalishaji wa kusafisha mafuta.
Forum