Kampuni hiyo ambayo inasambaza takwimu kwa makampuni mbalimbali kwa madai ya watu kufanyishwa kazi kwa nguvu katika mkoa wa Xinjiang ili kuwasaidia kufuata sheria za Marekani.
Wizara hiyo ya mambo ya nje ilisema Jumanne “itachukua hatua kukabiliana” na Kharon na mkurugenzi wake wa uchunguzi kwa kutoa “kile kinachoitwa ushahidi kwa vikwazo visisvyo halali vya Marekani kuhusiana na Xinjiang.”
Kampuni ya Kharon
Katika kujibu hilo, Kharon ambayo ina makao yake Los-Angeles ilisema haina uwepo nchini China, na hivyo hatua hiyo ilikuwa “kwa ujumla ni ishara” na haiwezi kuathiri operesheni zake au uwezo wake wa kuwahudumia wateja wake.
“Katika kuwahudumia wateja wetu na biashara zote za kimataifa ambazo zinataka kutekeleza programu maarufu za kudhibiti hatari, Kharon itaendelea kufanya utafiti na kutoa uchambuzi wa takwimu ambao hauegemei upande wowote, unajitegemea, na unatumia vyanzo vya kuaminika,” ilisema katika taarifa yake.
Mtafiti wa zamani wa Taasisi ya Center for Advanced Defense Studies iliyoko Marekani pia atawekewa vikwazo.
Watu hao waliowekewa vikwazo watazuiliwa kuingia China, ikiwemo Hong Kong na Macau, na mali za Kharon nchini China zitazuiliwa, wizara hiyo ilisema.
Kharon ilisema makampuni yanategemea takwimu zake za nguvu kazi ya kulazimishwa kuweza kufuata Sheria ya Uyghur Forced Labor Prevention Act (UFLPA).
Sheria ya Marekani
Sheria hiyo ilisainiwa kuwa Sheria ya Marekani mwaka 2021 kuzuia kwa bidhaa ambazo zinatengenezwa na makampuni yaliyoorodheshwa kutoka katika mkoa wa Xinjiang, China mpaka wathibitishe kuwa wao hawazalishi bidhaa kwa kutumia au kufungamana na ajira za kulazimishwa.
Mwezi huu Marekani imezuia uingizaji wa bidhaa kutoka kampuni nyingine tatu ikiwemo Sichuan Jingweida Technology Group, ambayo huko nyuma iligunduliwa na Kharon kushiriki katika kuhamisha nguvu kazi mwaka 2017 ambapo maelfu ya wafanyakazi walipelekwa kufanya kazi katika viwanda mbalimbali.
Maafisa wa Marekani
Maafisa wa Marekani wanasema wanaamini mamlaka nchini China zimefungua kambi kadhaa za Wauyghurs na vikundi vingine vya Waislamu waliowachache huko Xinjiang. Beijing inakanusha kuhusika na unyanyasaji wa aina yoyote.
Vikwazo vinavyohusiana na Xinjiang vimejikita katika “uongo” na “maelezo ya uongo,” kulingana na Beijing, ambayo inasema Marekani imekazana kuiharibu utulivu uliopo Xinjiang na kuzuia maendeleo ya China.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters. Imechangiwa na waandishi wa VOA.
Forum