Uchaguzi wa Taiwan wa rais na bunge wa Januari 13 unafanyika wakati ambapo China inakiona kisiwa hicho kuwa himaya yake, ikiilazimisha Taiwan kukubali madai ya china.
Taiwan mapema mwezi Desemba, iliishutumu China kwa kulazimisha kiuchumi na uingiliaji kati, baada ya Beijing kutangaza kuondoa ushuru kwenye baadhi ya bidhaa za kemikali zinazoagizwa kutoka kwenye kisiwa hicho, ikisema kuwa Taipei ilikiuka makubaliano ya kibiashara yaliyofikiwa mwaka 2010 kati ya pande hizo mbili.
Hilo limekuja baada ya China kusema imebaini kuwa Taiwan iliweka vikwazo vya kibiashara kinyume cha sheria za Shirika la Kimataifa la Biashara, WTO, na makubaliano ya wa biashara ya 2010.
Forum