Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 07:39
VOA Direct Packages

China yaripotiwa kushuhudia baridi isiyo ya kawaida


Mwanaume akipita kwenye maji ya bahari yalioganda kutokana na baridi mjini Beijing, China. Desemba 22, 2023.
Mwanaume akipita kwenye maji ya bahari yalioganda kutokana na baridi mjini Beijing, China. Desemba 22, 2023.

Mji mkuu wa China wa Beijing umevunja rekodi kufuatia saa kadhaa za baridi iliyopita chini ya nyuzi sifuri katika mwezi wa Desemba, mara ya mwisho kwa hilo kutokea ikiwa ni 1951, pale baridi kali ilipokumba taifa hilo na kuweka historia.

Kaskazini na kaskazini mashariki mwa China kumeshuhudia baridi ya kihistoria tangu wiki iliyopita, wakati baadhi ya maeneo ya kaskazini yakishuhudia nyuzi 40 chini ya sifuri Celsius au hata zaidi, wakati upepo wenye baridi ukiendelea kuingia kutoka Arctic.

Kufikia Jumapili, kituo cha uangalizi mjini Beijing kilikuwa kimerekodi zaidi ya saa 300 za baridi ya chini ya sifuri, kuanzia Desemba 11, ukiwa muda mrefu zaidi tangu hali sawa na hiyo kushuhudiwa 1951, kulingana na gazeti la serikali la Beijing Daily.

Gazeti hilo limeongeza kusema kwamba Biejing imeshuhudia siku 9 mfululizo za nyuzi 10 chini ya sifuri Celsius ndani ya kipindi hicho. Miji kadhaa kwenye jimbo la kati mwa China la Henan, kusini magharibi mwa Beijing pia inashuhudia baridi kali, wakati mtambo wa kuzalisha umeme uliyopo mjini Jiaozuo ukijitahidi kuhakisha huduma zinapatikana ili kukabiliana na hali hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG