Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 07:49

China yaanza kujenga nyumba za muda kwa ajili ya manusura wa tetemeko la ardhi


Tetemeko la Ardhi nchini China
Tetemeko la Ardhi nchini China

Picha na Shirika la Xinhua News Agency, Mamia ya nyumba za muda zimejengwa siku ya Ijumaa (Desemba 22) kwa ajili ya manusura wa tetemeko la ardhi katika jimbo la kaskazini-magharibi la China la Gansu, Dec. 21, 2023.
Picha na Shirika la Xinhua News Agency, Mamia ya nyumba za muda zimejengwa siku ya Ijumaa (Desemba 22) kwa ajili ya manusura wa tetemeko la ardhi katika jimbo la kaskazini-magharibi la China la Gansu, Dec. 21, 2023.

Mamia ya nyumba za muda zilikuwa zikijengwa siku ya Ijumaa (Desemba 22) kwa ajili ya manusura wa tetemeko la ardhi katika jimbo la kaskazini-magharibi la China la Gansu, kulingana na shirika la utangazaji la serikali CCTV.

Tetemeko hilo la kiwango cha 6.2 kwa kipimo cha rikta lililotokea mapema saa sita usiku Jumatatu liliua zaidi ya watu 130 katika majimbo ya Gansu na Qinghai, kujeruhi karibu 1,000 na kuwaacha walionusurika wakikabiliwa na hali ya sintofahamu kwa miezi kadhaa bila makazi ya kudumu.

Huko Gansu, zaidi ya nyumba 207,000 ziliharibiwa na karibu nyumba 15,000 zilianguka, na kuwaathiri zaidi ya watu 145,000, kulingana na vyombo vya habari vya ndani. Zaidi ya bidhaa 128,000 za dharura yakiwemo mahema, vitambaa, taa za mahema na vitanda vimewasilishwa pamoja na vyakula kwa waathirika.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG