Watetezi wa mazingira wameliambia shirika la habari la AP wao pia wana wasiwasi kuwa kampuni hiyo, The Blue Formula, inawezekana wanauza samaki ambao wanavuliwa kinyume cha sheria.
Bidhaa hiyo, ambayo kampuni hiyo inaielezea kuwa “siri bora ya asili iliyosalia,” ni kipaketi kidogo cha unga wenye collagen inayotolewa kutoka katika samaki huyo na imetayarishwa ili kuchanganywa katika kinywaji.
Kwa mujibu wa Mkataba wa Kimtaifa wa Biashara katika Viumbe Vilivyo Hatarini vya Fauna na Flora, ambao Mexico na Marekani wote wametia saini, uuzaji wowote wa samaki aina ya totoaba ni kinyume cha sheria, isipokuwa iwapo atazalishwa katika himaya kwa kibali maalum. Ikiwa ameorodheshwa katika viumbe vinavyolindwa, uuagizaji wa kibiashara wa samaki huyo ni kinyume cha sheria chini ya sheria ya biashara ya Marekani.
Kikundi cha waangalizi wa mazingira cha Cetacean Action Treasury kiliitaja kampuni hiyo mwezi Novemba. Baadaye siku ya Alhamisi, muungano wa mashirika ya hisani ya mazingira – The Center for Biological Diversity, National Resources Defence Council na Animal Welfare Institute – ulituma malalamiko ya maandishi kwa taasisi ya CITES.
Kampuni ya Blue Formula haikujibu ombi la shirika la habari la AP likiwataka maoni yao.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.
Forum