Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 10:12

Tanzania: uvuvi wa samaki kujadiliwa


Samaki akiwa amevuliwa kutoka kwenye maji ya bahari
Samaki akiwa amevuliwa kutoka kwenye maji ya bahari

Kulingana na makamu mkuu wa chuo kikuu cha DSM kilichoandaa kongamano hilo Profesa Rwekaza Mkandala, huu ni mkutano wa 16 na unafanyika kwa mara ya kwanza katika eneo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Wataalamu kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika wameanza mkutano wao wa siku nne jijini dar es salaam nchini Tanzania kujadili kile kinachoitwa uchumi wa uvuvi wa samaki ambao unaripotiwa kukua kwa kasi lakini ukiandamwa na changamoto ya kushamiri kwa uvuvi haramu.

Zaidi ya wataalamu 200, waliobobea kwenye masuala ya mazingira, elimu ya viumbe vya kwenye maji na uchumi endelevu wameanza kunoa bongo wakisaka majibu ya kukwamua sekta hiyo ambayo ripoti inaonyesha inakuwa kwa kasi mno.

Kulingana na makamu mkuu wa chuo kikuu cha DSM kilichoandaa kongamano hilo Profesa Rwekaza Mkandala, huu ni mkutano wa 16 na unafanyika kwa mara ya kwanza katika eneo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Tanzania pekee inatajwa kuingiza kiasi cha dola za kimarekani milioni 500 kila mwaka kutokana na sekta hiyo ya uvuvi. Kama alivyobainisha mtaalamu mmoja kwenye kongamano hilo, Dr Paul Onyango mkutano huo unatoa fursa ya kuzijadilia rasilimali zinazopatikana baharini.

Pamoja na sekta hii ya uvuvi kuchangia pakubwa kwenye uletaji maendeleo kwa kila taifa hata hivyo kuna mkwamo mmoja unaosalia ambao unazusha kitisho cha kutowesha kwa baadhi ya viumbe. Meeneo mengi ya bahari yanakabiliwa na ongezeko la uvuvi haramu linalochangizwa na shughuli za kimagendo.

Hata hivyo kulingana na Naibu waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Benedict Ole- Nangoro serikali inachukua hatua kadhaa kukabiliana na hali hiyo.

Mwishoni mwa mkutano wao, wataalamu hao wamepanga kuweka maazimio kadhaa yatayosaidia kuikwamua sekta hii ya uvuvi

XS
SM
MD
LG