Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 13:09

Rais Xi Jinping wa China amekutana na viongozi wa Vietnam mjini Hanoi

Waziri Mkuu wa Vetnam Pham Minh Chinh, (Kulia) akizungumza na Rais wa China, Xi Jinping (Kati-kati Kushoto) huko Hanoi, Dec. 13, 2023.
Waziri Mkuu wa Vetnam Pham Minh Chinh, (Kulia) akizungumza na Rais wa China, Xi Jinping (Kati-kati Kushoto) huko Hanoi, Dec. 13, 2023.

Pande hizo mbili zilisaini makubaliano kadhaa, yaliyojikita katika kuimarisha ushirikiano, ikijumuisha kufanya kazi pamoja kwa ajili ya maendeleo ya reli na mawasiliano.

Rais Xi Jinping wa China amekutana na viongozi wa Vietnam katika siku ya pili ya ziara yake mjini Hanoi, kufuatia hatua ya Vietnam kuimarisha uhusiano na Marekani na Japan.

Xi alizungumza kwanza na Mwenyekiti wa Bunge la Taifa la Vietnam, Vuong Dinh Hue, kabla ya kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Vietnam, Pham Minh Chinh, na Rais Vo Van Thuong.

Pande hizo mbili zilisaini makubaliano kadhaa, yaliyojikita katika kuimarisha ushirikiano, ikijumuisha kufanya kazi pamoja kwa ajili ya maendeleo ya reli na mawasiliano.

Viongozi hao pia walikubaliana mabadilishano ya wafungwa, ingawa maelezo machache yalitolewa kuhusu makubaliano hayo.

Pia walikubaliana kutathmini tena mkataba ulioisha muda wake mwaka 2020, kulingana na vyombo vya habari vya ndani, ambao unaruhusu doria ya pamoja katika Ghuba ya Tonkin ambayo iko kati ya jimbo la kusini mwa kisiwa cha China cha Hainan na pwani ya kaskazini mashariki ya Vietnam.

Forum

XS
SM
MD
LG