Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 03:43

Uokoaji unaendelea katika maeneo yaliyoathiriwa na Kimbunga Ian Florida


Maafa yaliyoachwa na Kimbunga Ian Florida.
Maafa yaliyoachwa na Kimbunga Ian Florida.

Watu wakitumia mitumbwi katika mitaa ambayo ilikuwa inapitika siku moja au mbili kabla.  Maelfu hawana umeme. Helikopta za Walinzi wa Taifa zikiruka kuwaokoa wakazi waliokwama katika visiwa vilivyozingirwa na maji Florida.

Siku kadhaa baada ya Kimbunga Ian kupita na kuharibu maeneo ya Florida hadi North and South Carolina, hatari inaendelea kuwepo, na hata hali kuwa mbaya zaidi katika baadhi ya maeneo. Ilikuwa ni dhahiri kuwa njia ya kuleta afueni kutokana na dhoruba hii ni ndefu na yenye maumivu.

Ian bado haijamalizika. Kimbunga hicho kimeelekea Virginia na kuleta mvua Jumapili na maafisa wametahadharisha uwezekano wa mafuriko makubwa kutokea katika pwani hiyo, huku kukiwa na ilani ya mafuriko iliyotolewa Jumatatu.

Mabaki ya Ian yalisogea ufukweni na kujenga dhoruba ya nor’easter ambayo inatarajiwa kuongeza maji zaidi katika Ghuba ya Chesapeake iliyosongwa na maji mengi na ilitishia kusababisha mafuriko yenye mawimbi makubwa huko katika mkoa wa Virginia Hampton Roads kwa miaka 10 hadi 15 iliyopita, alisema Cody Poche, mtabiri wa hali ya hewa wa Taifa.

Uharibifu ulioachwa na Kimbunga Ian eneo la Pine Island, Florida.
Uharibifu ulioachwa na Kimbunga Ian eneo la Pine Island, Florida.

Maeneo mengine ya pwani ya yanaweza kujionea mawimbi ya kina cha juu kuliko kawaida. Mji wa kisiwani wa Chincoteague huko Virginia ulitangaza hali ya hatari Jumapili na kuwashauri wakazi katika baadhi ya maeneo waondoke.

Ufukwe wa Mashariki na sehemu ya kaskazini ya Outer Banks huko North Carolina kulikuwa na uwezekano wa kuathiriwa.

Takriban watu 68 wamethibitishwa kufariki: 61 huko Florida, wanne North Carolina na watatu Cuba.

Huko Florida, Meya Ray Murphy wa eneo la Fort Myers Beach alikiambia kituo cha televisheni cha NBC katika kipindi cha “Today Show” Jumatatu kuwa shughuli za kutafuta na uokoaji zitaendelea kwa siku kadhaa zijazo.

Murphy alisema ndiyo maana wakazi walioondelewa wengi wao wamewekwa maeneo ya mbali na makazi yao.

Huku idadi ya vifo ikiongezeka, Deanne Criswell, Mkuu wa Shirika la Kusimamia shughuli za dharura la serikali kuu (FEMA) alisema serikali kuu ilikuwa tayari kusaidia kwa kiwango kikubwa, ikijikita kwanza kuwasaidia waathirika huko Florida, iliyoathiriwa zaidi na moja ya vimbunga vikali kabisa ambacho kimetokea Marekani

Rais Joe Biden na mkewe Jill Biden wamepanga kutembelea jimbo hilo Jumatano.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP

XS
SM
MD
LG