Ian kiligonga mkoa wa Pinar del Rio nchini Cuba, ambapo serikali iljenga makazi 55 ya muda kuwahamisha watu 50,000, kuwapeleka wafanyakazi wa dharura kwenye maeneo yaliyoathiriwa, na kuchukua hatua za kulinda mazao katika eneo linalokuza tumbaku nyingi zaidi nchini humo.
Kituo cha Kitaifa cha Vimbunga cha Marekani kilisema Cuba iliathiriwa pakubwa na upepo na dhoruba wakati kimbunga hicho kilipopiga, kikiwa na upepo wa kasi ya kilomita 205 kwa saa.
Kimbunga Ian kilitarajiwa kupata nguvu zaidi katika Ghuba ya Mexico, na kufikia kasi ya zaida ya kilomita 209 kwa saa, kinapokaribia pwani ya kusini magharibi mwa Florida, ambako watu milioni 2.5 waliamriwa kuhama makazi yao.