Ian inaweza kuwa kimbunga kibaya zaidi katika historia ya Florida,"Rais Joe Biden alisema baada ya dhoruba hiyo kuleta upepo mkali, na kugeuza mitaa kuwa mito inayotiririsha maji ambayo ilisomba nyumba na kuacha idadi isiyojulikana ya majeruhi.
Kulingana na uchanganuzi wa haraka na wa awali, mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na binadamu yaliongeza mvua kali ambayo Ian ilileta kwa zaidi ya asilimia 10, wanasayansi wa Marekani walisema.
Mabadiliko ya hali ya hewa hayakusababisha dhoruba lakini yalisababisha kuwa na mvua, nyingi zaidi" Michael Wehner wa Maabara ya Kitaifa ya Lawrence Berkeley, mmoja wa wanasayansi waliohusika na ugunduzi huo mpya alisema.