Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:31

UN yamtaka kiongozi wa juu wa utawala wa kijeshi Myanmar kujiuzulu


Jenerali Min Aung Hlaing
Jenerali Min Aung Hlaing

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Myanmar  siku ya Ijumaa  amemtaka kiongozi wa kijeshi wa nchi hiyo kujiuzulu na kurudisha madaraka aliyochukua kwa nguvu katika mapinduzi ya kijeshi Februari 1 kwa serikali iliyochaguliwa kidemokrasia.

“Sioni utulivu wala mustakbali mwema wa Myanmar chini ya uongozi wa amiri jeshi huyu na Tatmadaw,” Christine Schraner Burgener ameiambia kamati ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya haki za kibinadamu.

“Iwapo Jenerali wa Ngazi ya Juu Min Aung Hlaing anajali kikweli mustakbali wa nchi yake, ni lazima ajiuzulu na kukabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia kulingana na matakwa ya wananchi,” amesema.

Tatmadaw ni jin la jeshi la Myanmar.

Schraner Burgener alitoa wito huo katika muhtasari wake wa mwisho alioutoa Umoja wa Mataifa. Ataachia madaraka ifikapo Oktoba 31, baada ya kushikilia madaraka hayo kwa miaka mitatu na nusu.

Ametumia muda wa miezi tisa akikabiliana na mapinduzi yaliyofanywa na jeshi, ambayo yamefanya Myanmar kuingia katika vurugu na uvunjifu wa amani. Zaidi ya raia 1,100 wameuawa, na maelfu kufungwa jela na zaidi ya watu 250,000 kupoteza makazi yao.

Jeshi la Myanmar lilidai wizi mkubwa wa kura katika uchaguzi wa Novemba 2020, ambapo kiongozi asiyepingwa wa Chama cha National League for Democracy (NLD)Aung San Suu Kyi alishinda kwa kishindo.

Baada ya matokeo hayo jeshi lilimuweka kizuizini Suu Kyi, Rais Win Myint na viongozi wengine wa ngazi ya juu wa NLD na kuanza kuwakamata wanaoshiriki katika maadamano yaliyokuwa awali ya amani.

Jeshi hilo limepuuzia shinikizo la kimataifa kubadili hali hiyo, na mazingira yamezidi kuharibika. Ghasia zimeenea nchi nzima, na serikali ya Umoja wa Kitaifa ya NLD imeunda Jeshi lake la Ulinzi wa Wananchi.

XS
SM
MD
LG