Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:22

Wanamgambo wa Rohingya wadaiwa kufanya mauaji


Mwanaharakati wa Rohingya Mohib Ullah
Mwanaharakati wa Rohingya Mohib Ullah

Kaka wa kiongozi wa jumuiya ya Warohingya, Mohib Ullah, aliyeuwawa amewalaumu wanamgambo kwa kufanya mauaji ya kaka yake katika kambi ya wakimbizi nchini Bangladesh kwa sababu ya umaarufu wake, na kazi yake ya kutetea haki za binadamu.

Mohib Ullah alionekana katika miaka ya hivi karibuni kama mmoja wa watu mashuhuri zaidi anayewakilisha Warohingya 850,000 ambao wamekwama katika makambi nchini Bangladesh baada ya kukimbia ghasia nchini Myanmar mwaka 2017.

FILE - Mohib Ullah, kiongozi wa jumuiya Rohingya, akihutubia sherehe za kumbukumbu ya mwaka wa pili wa mashambulizi yaliyofanywa na jeshi iliyosababisha kundi kubwa la watu kukimbia kutoka Myanmar kwenda Bangladesh, katika kambi ya wakimbizi Kutupalong huko Ukhia.
FILE - Mohib Ullah, kiongozi wa jumuiya Rohingya, akihutubia sherehe za kumbukumbu ya mwaka wa pili wa mashambulizi yaliyofanywa na jeshi iliyosababisha kundi kubwa la watu kukimbia kutoka Myanmar kwenda Bangladesh, katika kambi ya wakimbizi Kutupalong huko Ukhia.

Watu wasiojulikana wakiwa na bunduki walimuua Jumatano jioni, na kusababisha serikali ya Bangladsh kupeleka mamia ya polisi zaidi katika makambi ya wakimbizi hao Alhamisi.

Takriban watu 25,000 walihudhuria sala ya mazishi yake katika kambi kuu ya Kutpalong Alhamisi, kwa mujibu wa polisi.

Lakini kiongozi mwingine wa Warohingya Nazir Hossain anasema waliohudhuria walikuwa 200,000.

Habib Ullah ameiambia AFP kwamba katika miezi ya hivi karibuni kaka yake alipata vitisho vya kuuawa kutoka kwa jeshi la uokovu la Arakan Rohingya na kwamba takriban wanaume wanane kutoka kundi hilo walihusika katika shambulizi hilo.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la Habari la AFP

XS
SM
MD
LG